WAZIRI AWESO KUKUTANA NA WADAU SEKTA YA MAJI ARUSHA

...............

Waziri wa Maji Jumaa Aweso anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa wadau wa sekta ya maji utakaofanyika kwa siku mbili jijini Arusha.

Mkutano huo utafanyika kuanzia tar 13 hadi 14 mwezi huu katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC  jijini Arusha ambapo watashiriki Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Jamal Katundu,Naibu Waziri wa Maji MarryPrisca Mahundi pamoja  na wadau mbalimbali.

Imeelezwa dhumuni la mkutano huo ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuwashukuru wadau mbalimbali wa sekta ya maji kwa jitihada wanazozifanya za kuwezesha upatikanaji wa maji nchini.

Aidha watapongezwa kwa mchango wao mkubwa wa hali na mali katika kuwezesha mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya maji nchini.

 Sambamba na hilo, wadau hao watapewa fursa ya kujadili, kutoa maoni na mapendekezo kwenye Rasimu ya Sera ya Taifa ya Maji ya Mwaka 2002 Toleo la Mwaka 2023 na Mpango Mkakati wa Wizara.

0/Post a Comment/Comments