Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania Dkt. Erasmus Kipesha akitoa Elimu kwa mdau aliyetembelea banda la TEA wakati wa maonesho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mnazi Mmoja.
Hamza Hassan (Mwenye tisheti nyeupe) Afisa Utafutaji Rasilimali akifafanua jambo kwa mdau wa Elimu aliyetembelea banda la TEA katika Maonesho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (TEA) Mwanahamisi Chambega, katika maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Chambega amesema, Faida ya kuchangia kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa ni pamoja na wachangiaji kutangazwa na kutambuliwa kitaifa, ambapo mchangiaji huandikwa katika rejesta ya kudumu ya wachangiaji wa elimu.
Amesema faida nyingine ni kupata Hati ya Utambuzi wa Uchangiaji wa Elimu (Certificate of Educational Appreciation ambapo mchangiaji anaweza kuitumia kuomba nafuu ya kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (1) cha Sheria ya Kodi ya Mapato Sura 332 marejeo ya mwaka 2019.
Aidha, mchangiaji anaweza kuwa mtu yeyote anayetoa udhamini au ruzuku kwa wanafunzi mbali na watoto wake, familia yake au mwajiri wake, kwa lengo la kuwasaidia kuendelea na elimu kwenye ngazi ya sekondari au elimu ya juu ambapo udhamini huo atautoa kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi Masozi Nyirenda amesema kuwa kuanza kutumika kwa sera mpya ya elimu na mafunzo kutasaidia wanafunzi kuhitimu wakiwa na ujuzi ambao utawawezesha kujiajiri na kuajiriliwa.
Amesema TEA kupitia mfuko wa kuendeleza ujuzi SDF, umeshafikia vijana zaidi ya 49,000 ambao wamepata ujuzi kwenye fani mbalimbali za kimkakati hivyo kuanza kwa sera hiyo hapo mwakani itasaidia kuwafikia vijana wengi zaidi.
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) inalo jukumu la kuhamasisha uchangiaji maendeleo ya Elimu kote nchini ambapo, kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Elimu, Namba 8 ya mwaka 2001 sehemu ya 12 (1) (a) na (b) mchangiaji ni mtu yeyote anayetoa mchango wa pesa, bidhaa, au huduma kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa au kutekeleza mradi kwa uratibu wa Mfuko huo wa Elimu.

.jpg)

.jpg)


Post a Comment