COSTECH YAWATAKA WATAFITI KUTUMIA FURSA ZINAPOJITOKEZA

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu (kulia) wakati akizungumza na waandishi wa habari , Jijini Dar es Salaam kuhusu ufadhili wa miradi ya utafiti kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.Afisa Mratibu Mwandamizi wa Utafiti COSTECH, Neema Tindamanyire, akizungumza na waandishi wa habari, Jijini Dar es Salaam akielezea namna ya watafiti watakavyoshiriki katika warsha itakayofanyika kwa njia ya Mtandao a kuhusu ufadhili wa miradi ya utafiti kwa ajili ya  kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi

.....................

Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) inatarajia kuingia makubaliano na serikali ya Sweden (SIDA) mwezi Februari mwaka huu kwa ajili ya kufadhili shughuli za Sayansi,Teknolojia na ubunifu (STU) kwa kipindi cha Miaka mitano ijayo.

Imeelezwa kuwa huo ni muendelezo wa makubaliano ambayo Tume hiyo ilisaini na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Nchini Norway,Norad kwa lengo la kutekeleza program ya utafiti wa mabadiliko ya tabia nchi kwa Miaka mitano ijayo.

Hayo yamebainishwa  leo na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH,Dkt Amosi Nungu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa utekelezaji wa program hiyo unategemea kuchangiza sekta ya Sayansi na Teknolojia kwa kuleta Teknolojia bunifu na Elimu ya kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha Dkt Nungu amewataka watafiti kuunda timu ya watafiti ambao wamebobea kwenye maeneo yao lakini pia kujenga uwezo wa watafiti wachanga.

"Program hii ilizinduliwa tar 11/10/2023  na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt Suleiman Jaffo kwa kuwa masuala ya mazingira yanasimamiwa na Wizara yake na hivyo COSTECH ni mratibu wa utekelezajiwa program hii ambayo inatekelezwa Tanzania Bara na Visiwani"amesema Dkt Nungu

Amesema kuwa miradi itakayofadhiliwa ni miradi mikubwa ambapo Kila mradi unategemewa kugharamiwa kwa Kati ya Takriban Shilingi za kitanzania milioni mia Moja na Ishirini hadi milioni mia sita kwa muda wa Miaka minne.

Akizungumza umuhimu wa warsha mtandayo ambayo imeandaliwa na COSTECH,Afisa Mratibu Mwandamizi wa Utafiti Neema Tindamanyire amesema kuwa ni pamoja na kujibu maswali kutoka kwa watafiti Ili waweza kuelewa na kundika machapisho mbalimbali.

Katika Hatua nyingine,Tume hiyo imeandaa warsha itakayofanyika kwa njia ya Mtandao Kesho Aprili 1,2024 kwa lengo la kujenga ufahamu na uelewa zaidi kwa watafiti Ili waweze kuandaa Maandiko mazuri na shindani.

0/Post a Comment/Comments