Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam.
NA MUSSA KHALID
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanikiwa kumkamata Kinara wa Mtandao wa Wafanyabiashara wa Dawa za Kulevya aina ya Cocaine katika eneo la Kinondoni jijini Dar es salaam ambaye alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas Lyimo amesema pia Mamlaka hiyo imekamata jumla ya gramu 692.336 za Cocaine zinazowahusisha watuhumiwa wanne katika Operesheni maalum zinazoendelea nchini.
Kamishna Jenerali Lyimo amesema mfanyabiashara wa wa Mtandao huo alikamatwa sambamba na washirika wake watatu ambapo Kati yao wawili wamekamatwa jijini Dar es salaam na Moja amekamatwa Kijiji cha Shamwengo Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya.
Aidha Lyimo amesema Dawa ya Kulevya aina ya Cocaine huzalishwa kwa wingi katika Bara la Amerika ya Kusini na husafirishwa kwa njia ya anga na wawebaji maarufu punda kwa kuzimeza katika mfumo wa pipi Kuanzia gramu 300 hadi1200 huku baadhi yao wakaibeba gramu 3000 kwa wakati mmoja.
"Dawa ya Kulevmyya aina ya Cocaine inazalishwa kutoka kwenye mmea wa Coca unaojulikana kitaalamu Erythroxylum coca ambayo hulimwa zaidi katika nchi za Bolivia,Peru na Colombia zilizopo Amerika ya Kusini ambapo ni hatari sana kwa afya ya mtumiaji kwani huathiri utendaji wa mfumo wa fahamu,husababisha kukosa usingizi,shinikizo la Damu,magonjwa ya moyo,Kiharusi na vifo vya Ghafla" Amesema Lyimo
Lyimo amesema pia Cocaine inaweza kusababisha matatizo ya afya ya akili na husababisha hasira,ukatili,vurugu,kukosa utulivu na hata mtumiaji kutaka kujiua.
Hata hivyo Mamlaka hiyo imesema itafanya Operesheni Kali za nchi kavu na baharini kwa mwaka huu 2024 ambapo zitahusisha mashamba ya Dawa za Kulevya,kwenye mipaka,maeneo ya mijini na hata vijiwe vya usambazaji na watumiaji wa Dawa za Kulevya
Mamlaka hiyo imetoa onyo kwa watakaoendelea kujihusisha na uzalishaji ,biashara na matumizi ya dawa za kulevya hapa nchini kuacha kwani serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania I meendelea kuiwezesha Mamlaka kwa kununua vifaa vya kisasa na mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka.
Post a Comment