DIAGEO SBL KWENYE KASHFA YA UKWEPAJI KODI WA MUDA MREFU?

...................,...
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji wa Bia, Diageo Serengeti Breweries Limited (SBL), ambayo ni moja ya kampuni kubwa nchini, imekuwa ikikwepa kodi kwa muda mrefu ili kupata faida kubwa, uchunguzi wabaini.

Taarifa ya "Diageo Serengeti Breweries Tanzania - The Insider Story –Sehemu ya 1" inasema kwamba Deloitte Due Diligence Tanzania ilikagua mahesabu ya Diageo SBL kati ya Januari 2009 na Oktoba 2010 na kubaini upungufu mkubwa katika mikataba ya ajira, kodi ya zuio, kodi ya faida ya mapato ya kampuni, kodi ya ongezeko la thamani (VAT), ushuru wa biashara na kodi ya mapato yatokanayo na ajira (PAYE).

Hasa, taarifa inaonyesha ukwepaji kodi kwa kodi ya mapato yatokanayo na ajira tu ilifikia takribani $2.4 milioni kwa mwaka, hali ambayo iliendelea kwa miaka mingi tangu mwaka 2001 hadi 2010.

Mikataba ya wafanyakazi wandamizi inaonyesha kiasi cha fedha za Kitanazania, wakati orodha ya wakopea mshahara huonyesha kiasi tofauti kwa kulinganisa na kile kilichoko kwenye mikataba.

Uchunguzi unaonyesha Diageo SBL ilikuwa ikitumia aina mbili za mikataba ya ajira kwa wafanyakazi kutoka nje ya nchi na wafanyakazi waandamizi ambao ni Watanzania.

Aina moja ya mshahara (kurasa 3 tu) unaonyesha mshahara wa uwongo ambao ni wa chini katika shilingi za Tanzania – aina hii ya mikataba ndiyo hutumika kuwaonyesha maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania

(TRA), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)na kwa mchakato wa kupata kibali cha kazi, wakati aina nyingine mkataba wenye ukurasa wa ziada (kurasa 4) ukionyesha mshahara kwa Dola za Kimarekani ukifichwa.

 

Zaidi ya hayo, aliyekuwa Mdhibiti wa Fedha za Kampuni ya Diageo SBL, Bw Harish Kumar alithibitisha ukaguzi wa mahesabu ya kampuni yaliyokwishakaguliwa ulifanyika tena na Kampuni ya Price Waterhouse Coopers kuanzia mwaka 2006 hadi 2010 na kuthibitisha ukaguzi uliofanywa na Kampuni ya Price Waterhouse Kenya na Kampuni ya Price Waterhouse Tanzania.

 Bw Kumar aliahidi kutuma barua pepe kuonyesha hesabu hizo,lakini baadaye alipotafutwa kwa simu hakupatikana na tulipojaribu kumtafuta tena hakupatikana.

Kwa nini ukaguzi wa mahesabu ya Diageo SBL uliofanywa, kwa mujibu wa Deloitte Due Diligence, ni kwa mwaka 2009 na 2010 (miezi 20)? Ukaguzi wa ulipaji kodi kwa miaka iliyotangulia tangu mwaka 2001 ulifanywa lini? Ni kwa jinsi gani Diageo SBL, East African Breweries walifikia tathmini ya haki?

Ni nini lilikuwa hitaji la kukagua tena mahesabu yaliyokwisha kaguliwa na TRAkwa miaka 2006 hadi 2010 na PWC, na kufanywa na PWC Tanzania?

Hitaji la kukagua tena mahesabu kutoka 2006 hadi 2010 naPWC linaonyesha “mapato ya kweli ya biashara” ya Diageo SBL kwamba huenda ukaguzi wa awali haukuzingatia vigezo vya ukaguzi au haukutoa picha halisi ya mahesabi au ulifanyika kwa hila ili kuonyesha “mahesabu yalikuwa sahihi”?

Hapa ni kampuni ambayo ilikuwa na umiliki wa soko la asilimia 8-10mwaka 2009.

Nini maana ya umiliki wa soko? Umiliki wa soko – unakokotolewa kwa utumiaji mzima wa soko la bidhaa mahususi kwa kugawa kwa mauzo yote ya bidhaa zinazofanana kwa kipindi maalumu.

Kutokana na mahesabu yaliyokaguliwa na TRA, kwa nini Diageo East African Breweries ililipa £60 milionikwa kitegauchumi cha asilimia 51kwa Diageo SBL, ambayo kwa sasa ni asilimia 85?

 

Kwa maneno mengine,kwa jinsi gani Diageo East African Breweries ilifikia kwenye tathmini ya umiliki wa soko wa haki? Mtu mwingine angeweza kusema kwamba Diageo SBL ina thamani ya chapa.

Hata hivyo,thamani ya chapa kwa asilimia ya 8-10 ya umiliki wa soko? Hisa zisizo na riba ya kudumu za chapa nzuri zinapibwa kwa njia mbili, kwa wingi na kwa ubora.

Kipimo cha wingi ni pamoja na kupima mapato, faida, hasara, na mauzis. Methodolojia ya ubora wa kipimo ni pamoja na sababu zisizoweza kueleweka kwa urahisi kama vilekuridhika kwa watumiaji, ufahamu wa watumiaji, kufahamika kwa chapa, nk.

Kama kuna tofauti kati ya ukaguzi wa mahesabu uliofanywa na TRA na ule wa PWC, kama ni ndiyo, ni nini kilitokea kwa kodi ambayo haikulipwa kuanzia mwaka 2006 hadi 2010?

Taarifa ya DeloitteDue Diligence ilikuwa kwa miezi 20 (mwaka 2009 hadi mwaka 2010) ambayo inaonyesha maeneo ambayo kodi ilikwepwa, ni nini kilitokea kuanzia mwaka 2001 hadi 2008?

Kiasi cha jumla kilicholipwa ni kama asilimia 85ya hisa zisizo na riba ya kudumu za Diageo SBL ni zaidi ya $150 milioni hadi sasa, ni nini kilitokea kwa kodi ya faida ya mtaji?

Uchunguzi – Shauri Mahakamani

Uchunguzi kuhusu kuachishwa kazi kwa aliyekuwa Meneja Mkuu na Mkuu wa Rasilimali Watu, Dk Hector Sequeirawa Diageo SBL,aliyeletwa

Tanzania mwaka 2008, unaonyesha ulisababishwa na kukataa kusaini waraka/mkataba wowote wa ajira ambao ulikuwa unaipunja Serikali ya Tanzania.

Hata hivyo, Diageo SBL inadai mamlaka za Uhamiaji na Ajira hazikuhuisha kibali chake cha kazi, jambo ambalo ushahidi mbele Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Mahakama Kuu ya Tanzania ulionyesha ni wa uwongo.

"Mjibu mashtaka hakutoa ushahidi wowote kwamba baada ya kuvunja mkataba wa mlalamikaji walitangaza tena nafasi yakeili ijazwe na wabobezi wenyeji. Ushahidi wao kwamba ilikuwa nafasi ya wenyeji, kwa hiyo, haina ushahidi wowote," inasomeka sehemu ya hukumu.

Cha ajabu nafasi ya Dk Sequeirailichukuliwa na raia wa Ghana– aliyejulikana kamaEric Adedevoh na baada ya kuhamishwa raia wa Afrika Kusini Bi Arleen Abrahams, ambayo ilitolewa ushahidi mbele ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

Sehemu hiyo ya hukumu ya CMA inasomeka tena kwamba, Mjibu Mashtaka asingeweza kuamua kuajiri watu wengine kutoka nje, yaani Bw Eric Adedevoh na baadaye Bi Arleen Abrahamskwa vile hawa wawili waliajiriwa baada ya kusitisha mkataba wa kazi wa mlalamikaji, inashinda mantiki kwamba mlalamikiwa alitangaza nafasi kwa lengo la kumwajiri mfanyakazi mwenyeji.

Sehemu ya hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu Dk Sequeira inasomeka: "...Mahakama hii ina uamuzi wa uthibitisho katika katika jambo hili na bila mashaka kwamba kuvunja mkataba wa mlalamikiwa ulikuwa kuficha ukweli na kudanganyia kibali cha kazi.

Kwenye kumbukumbu hakuna uthibitisho wowote wa kimaandishi kutoka kwa Ofisi ya Kamishna wa Kazi au Waziri wa Kazi akimnyima mlalamikiwa kibali cha kazi kwa muda wa mkataba wake uliobakia.”

Ucheleweshaji wa Makusudi

Utaratibu wa kuendesha shauri kwa mujibu wa Sheria ya Kazi ya Tanzania haupaswi kuchukua zaidi siku 30 hadi 90 kwa usuluhishi,na siku 90 hadi 120 kwa uamuzi.

Hata hivyo,kulingana namashauri yanayosajiliwa, hitimisho halina budi kufanyika ndani ya miezi 8 hadi 12 tangu kusajili kwa shauri. Lakini shauri la aliyekuwa Meneja Mkuu na Mkuu wa Rasilimali Watu lilichukua miezi 78 jumla.

Shauri hili lilisajiliwa kwanza CMA Wilaya ya Temeke,ambapo lilichukua miezi 67 kwaDiageo SBL kuleta mashahidi 3.

Uchunguzi wetu unaonyesha kwamba Diageo SBL ilitumia ushawishi wake kuchelewesha shauriili kumchosha aliyekuwa Meneja Mkuu na Mkuu wa Rasilimali Watu. Mei 2014 iliripotiwa Makao Makuu ya CMA kwa kutokuwepo ulazima wa kuchelewesha shauri na shauri likahamishwa kutoka CMA Wilaya ya Temeke kwenda to CMA Wilaya ya Ilala.

Yatokanayo na Uchunguzi

Dk Sequeira ni shahidi wa ukwepaji wa kodi ambao hii kampuni imekuwa ikijihusisha nao kama nafuu yake ingeenda katika njia sahihi mwaka 2017/18.

TRA wangejua ni nini kilitokea na suala zima la ukwepaji kodi kama unavyoonyeshwa na taarifa ya Deloitte Due Diligence ungewekwa wazi. Hivyo, kumchosha Dk Sequeira kwa kupigania haki yake mbinu hii ya ucheleweshaji inafanyika.

Diageo SBL ni kampuni iliyoorodheshwa kwenye soko la hisa na inafanya kazi katika takribani nchi 150duniani, hivyo kuorodheshwa kwenye masoko mengi ya hisa duniani. Kila Mamlaka ya Mtaji wa Soko duniani yangetaka kuwauliza Diageo SBL juu ya sababu zao kwa kukwepa kodi kwa kiwango hiki, jambo ambalo lina athari kwa biashara ya kampuni nzima.

Kutokana na uchunguzi wa habari hii kama ilivyoonyeshwa hapa juu, swali la kujiuliza ni je, kama aina hii ya ukwepaji wa kodi ungeweza kutokeaUingereza, Marekani au nchi yoyote iliyoendelea, Diageo SBL ingeweza kuruhusiwa kufanya biashara kwa miaka 15 kama ushahidi

 

unavyoonyesha wa shauri hili? Kesi kama hii zingeweza kuwepo huku mamlaka husika Marekani zikiangalia? Je, ingeweza kuwa hivyo mamlaka husika zikiangalia Uingereza? Jibu lake ni HAPANA. Kwa nini itokee hivyo Tanzania?

Diageo SBL wanajua wazi kwamba mifumo na miundombinu Tanzania haiku vizuri kwa kulinganisha na Ulaya na Marekani, hivyo wanatumia nafasi hii, huku wakijua kwamba wanatumia nguvu yao ya kifedha na ushawishi kuficha ukwepaji wao wa kodi.

Diageo SBL wanatumia ucheleweshaji wa shauri hili mahakamani kuficha ukweli unaoweza kujulikana na wamefanikiwa kufanya hivyo kwa miaka 15 iliyopita na kama kutatokea taarifa kuwa Dk Hector Sequeira amepotea au ameuawa, jambo hili litakufa kifo cha kimya.Haki inayocheleweshwa ni sawa na haki inayokataliwa!

Alipotafutwa kuhusu Ripoti ya Delloitte , John Wanyacha , Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Serengeti alisema kwamba hiyo ni ripoti ya muda mrefu na hakuwepo kazini.

“hiyo ni ripoti ya muda mrefu name sikuwepo kazini na siwezi kusema chochote ni miaka mingi karibu 12 iliyopita siwezi kujua chochote,” alisema Wanyacha

Kuhusu , Dr Hector ambaye alikuwa Meneja Mkuu Rasilimali Watu , alisema kwamba hilo swala lipo mahakamani hawezi kulizungumzia kabisa

“hilo swala lipo mahakamani na wewe unajua hivyo siwezi kusema chochote ni jambo lipo mahakamani na wewe unajua hivyo,,” aliongeza


0/Post a Comment/Comments