..............................
Timothy Marko
MDAU wa Mpira nchini Haji Manara amewataka wasanii,Wanamichezo ,wanamziki kutumia Umarufu wao kutengeza Pesa.
Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam Haji Manara amesema kuwa anatarajia kumbrand mkewe Zainabu kupitia Anna colection ambapo amesisitiza mkewe huyo amekuwa maarufu kupitia filamu ya jua kali inayooneshwa na Azam tv.
"KATIKA kubrand kipaji chake Zainabu kuteng'eneza filamu kubwa ndani nje ya nchi,nitatumia utalaamu wangu wa promotion Zai yupo katika mikono salama".Alisema Haji Manara.
MDau huyo wa Mpira Haji Manara alisema kuwa nivyema wasani wa filamu kujijenga kiuchumi ,msitumie umarufu wenu pasipo kutengeneza Fedha.
Alisema kuwa Mchezaji Mpira wazamani wa Juventus Ronaldo ana utajiri wa Dola Bil 1anatumia umarufu wake kupata fedha.
"Wasanii wanamichezo tumieni umarufukupata hela"Asisitiza Haji Manara.
Kwa upande wake Mke wa Haji Manara Zailylissa amesema kuwa lengo kukuzasoko ubunifu nakuwa mbunifu bora wa Afrika.
Post a Comment