Wakazi wa Kijiji cha Mkata kilichopo Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro waliokua wakijihusisha na Shughuli haramu za uharibifu wa Maliasili za Hifadhi ya Taifa Mikumi kwa uuzaji wa mkaa unaotokana na miti ya asili iliyopo katika Hifadhi hiyo, Wametaja siri ya kutokomea kwa biashara hiyo baada ya Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW), kuwa wezesha wananchi kiuchumi.
Akizungumzia mafanikio ya mradi wa REGROW katika Kijiji cha Mkata, Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw. Revocatus Mwanakatwe ameeleza kuwa, hadi sasa, kuna vikundi 10 vimewezeshwa kiasi cha Sh 400,018,600/= kwa ajili ya maendeleo ya wanachi.
Ameeleza kuwa kutokana na uchumi wa wanachi wa Kijiji hicho kukuwa kwa kasi kutokana na Mradi wa REGROW tabia ya ujangili wa ukataji miti ovyo katika Hifadhi ya Taifa Mikumi umepungua sana na wanachi wanashindana kwa biashara halali huku wakiwa walinzi wa Hifadhi.
Bw. Daniel Gaspar ambaye ni mnufaika wa mradi wa REGROW, ameeleza kuwa hadi ameweza kumiliki Maduka Mawili makubwa, Chombo cha moto cha usafiri mashamba, ujenzi na kulea vyema familia yake.
Aidha licha ya miradi mingine ya vikundi vya COCOBA katika Kijiji cha Mkata, kupitia mradi wa REGROW wananchi wanaendelea na ujenzi wa Nyumba nne za kufugia kuku zenye zaidi ya thamani ya Milioni 12, huku kikundi kingine kikitarajia kupata zaidi ya bilioni moja kutokana na kilimo cha vitungu.
Post a Comment