********
Zanzibar. Msajili wa Hazina Tanzania Bara, Nehemiah Mchechu, amefanya ziara ya kikazi visiwani Zanzibar kwa kumtembelea Msajili wa Hazina wa Zanzibar, Waheed Muhammad Ibrahim Sanya.
Ziara hii ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano yaoiyotiwa saini April, 2023 kati ya ofisi hizo mbili yenye lengo la kuijengea uwezo Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar katika kusimamia Mashirika ya Umma kwa kutumia uzoefu wa muda mrefu wa ofisi ya msajili wa Hazina Tanzania Bara.
Katika mazungumzo yao, wasajili hao wamekubaliana, kuongeza weledi katika kusimamia mashirika kwa manufaa ya umma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia, kubadilishana wafanyakazi na uzoefu wa utendaji wa kazi kitaalam na kuwa kioo cha ufanisi wa utendaji kazi na kushiriki kikamilifu katika kudumisha Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar.
Pamoja na ziara ya kikazi, Mchechu pia yupo visiwani Zanzibar kushiriki katika maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Post a Comment