RC CHALAMILA AWAHAKIKISHIA WANA- DAR ES SALAAM KUWA MIUNDOMBINU YA MSINGI YOTE ILIYOHARIBIWA ITARUDISHWA KWENYE MAHALI PAKE HARAKA IWEZEKANAVYO".

...........,......

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila leo Januari 22, 2024 amewahakikishia wana-Dar es Salaam kuwa Miundombinu ya msingi yote iliyoharibiwa na mvua itarudishwa kwenye Mahali pake haraka iwezekanavyo

RC Chalamila ameyasema hayo katika Mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo katika Ofisi yake iliyopo Ilala Boma Jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa huyo amezitaja barabara na madaraja yaliyoharibiwa na mvua kuwa ni pamoja na Barabara ya Mtongani Kunduchi, Daraja la Mbweni JKT, Daraja la Mbopo, Daraja la Goba, Daraja la Makulunza, Daraja la Kivule, Daraja la Msumi, ambapo amesema wakandarasi tayari wapo kazini kuhakikisha huduma zinapatikana kwa haraka

Hata hivyo RC Chalamila amesema kuwa Dar es Salaam iko salama, HAIJAMEZWA na yaliyotokea ni ya kawaida ambapo Serikali ya Mkoa inaendelea kuyaratibu

Kuhusu waliojenga mabondeni Mkuu huyo wa Mkoa amewataka kuhama Mara moja kwani wanahatarisha maisha yao na pia madhara ya kuendelea kuishi huko ni makubwa Sana

Vile vile RC Chalamila amewapiga marufuku wote wanaofanya Shughuli za kibinadamu kando kando ya Mito na kusema baadhi ya barabara zilizovunjika au kusombwa kifusi chake ni kutokana na Shughuli za kibinadamu

Aidhaa, Mhe. Chalamila amesisitiza kuwa Kampeni kubwa ya Usafi ya tarehe 23-24 Januari, 2024 itaendelea Kama lilivyopangwa na si kampeni ya kisiasa hivyo isihusishwe na kuzuia maandamano ambapo vyombo vya dola vitafanya Usafi kwenye maeneo yao na maeneo ya barabara watafanya Usafi makandarasi, vikundi mbalimbali na wadau wengine wote lengo ni kuzuia magonjwa ikiwemo kipindupindu

Mkuu wa Mkoa ameongeza kuwa wazazi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kuwapeleka watoto wao shuleni na marufuku walimu kudai michango kwa watoto hao

Mwisho kabisa RC Chalamila ameelezea kuwa taarifa za vifo vya maji Kama zipo au hazipo anayepaswa kutoa taarifa hizo ni Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wataalamu wa Afya baada ya kufanya postmoterm ili kubaini

0/Post a Comment/Comments