*********
Timothy Marko
MAMLAKA ya Bandari Tanzania(TPA) imesema katika kipindi cha july hadi Disembar 2023 imeweza kusanya shilingi Bilioni 694 kutoka shilingi bilioni 594cha mwaka 2022 .
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Placduse Mbossa amesema kiasi hicho cha Makusanyo kimetokana kutokana na shena kubwa ya Mizigo na Miradi mbalimbali inayoendelea sambamba na Ongezeko la wateja wanao tumia Bandari hiyo.
"Shabaha yetu ilikuwa ni kuongeza mapato na kuongeza kasi ya Upokeaji mizigo,Sasa hivi shehena kubwa imeweza kupokelewa katika Bandari yetu ya Dar es Salaam ikiwemo Shehena ya miradi ya Reli".Alisema Mkurugenzi mkuu
wa Mamlaka ya Bandari Placduse Mbossa .
Mkurugenzi Mbossa amesema kuwa taratibu za kukabidhiana kwa baadhi ya gatti na kampuni ya kutoka falme zakiarabu (Dubai) Dp world zinaendelea nakusisitiza kuwa Shughuli zote za Bandari zitakuwa Chini ya Mamlaka hiyo.
Amesema kuwa Matarajio ya Muwekezaji huyo atakayepewa baadhi ya Gatt kuziendesha unatarajia katika robo ya Mwaka 2024 nakwatoa wasiwasi waandishi wa Habari kuwa atakapo anza muwekezaji huyo waandishi wa Habari wataarifiwa.
"Makabidhiano ya Shughuli za Banndari zinahitaji umakini mkubwa Sheria ya Bandari imempa haki TPAkuendesha Bandari "Aliongeza Mkurugezi Mbossa.
Mbossa alisisitiza kuwa Muwekezaji DP World ataendesha Gatt ya 4hadi ya 7 chini ya Usimamizi wa TPA.
"Sasa hivi mifumo yetu inasomana sambamba na mamlaka ya Mapato TRA ,hii imetuongezea wigo mpana wa utoaji Mizigo ikiwemoMagari bandarini "Alibainisha Mbossa.
Post a Comment