Timothy Marko.
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA)imekuwa mwenyeji wa Mkutano wa Makamishina wa kuu wa Mamlaka za Mapato za nchi za jumuhia ya Afrika Mashariki.
Akizungumza na waandishi wa Habari Kamishina wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata amesema mkutano huo unaoanza leo unatarajia kumalizika kesho ukiwa na lengo kujengea uwezo wakusanyaji wa Mapato wanchi hizi kuwezesha kuwa wakusanyaji bora wamapato ikiwemo kubadilishana taarifa,uzoefu na utalamu katika kusimia na kusanya Mapato ya Serikali kati yaNchi za jumuhia ya Afrika Mashariki.
" Katika kutimiza malengo hayo Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ni Mwenyeji wa Mkutano wa 51 wa Makamishina wa Makamishina wawakuu wa Mamlaka za Mapato za jumuhia ya Afrika Mashariki ambapo Mgeni rasmi ni Katibu Mkuu wizaraya Fedha Dk.Natu El maamry Mwamba"Alisema Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Nchini Alphayo Kidata.
Kamishina Kidata alisema Mkutano huo umebebwa na maudhui ya kuongeza ushirikiano wa kikanda ili kuboresha Makusanyo6 Endelevu.
Alisema kuwa lengo la uanzishwaji wa jukwaa hilo la makamishina wakuu wa jumuhia ya Afrika Mashariki nikuhakikisha nikuhakikisha wanakuwa na Mamlaka zilizouwanishwa na jumuishi katika usimamizi wa kodi.
"Hii yote inalenga kuwezesha Biashara sambamba nakuboresha Makusanyo ya Mapato na kukabiliana navitendo vya ukwepaji kodi vinavyoleta madhara katika juhudiza taasisi zetu pamoja na serikali katika ukusanyaji wa mapato"Aliongeza Alphayo kidata.
Aidha ,Kamishina kidata alisisitiza kuwa hatua hizo zitasaidia kuwepo kwa fedha za umma za kutosha ilikuwezesha ukuaji wakiuchumi wa kikanda.
Alibainisha kuwa, Mazungumzo hayo nimuhimu kwa nchi hizo katika kuhamasisha rasmali kupitia taasisi za kikodi katika kusaidia serikali za nchi hizo kutekeleza miradi ya kimaendeleo.
"Mamlaka hizi za mapato zinatakiwa kuwa naumoja ili kuleta ufanisi katika usimamizi na ukusanyaji wa mapato kuzuia ukwepaji kodi na kutoa huduma bora kwawalipakodi" Alieleza Kamishna kidata.
Post a Comment