........................
Timothy Marko.
Vyama visivyo na uwakilishi Bungeni vimewaomba Viongozi wasiasa nchini kutumia njia Sahihi ya kudai Mabadiliko ya Sheria uchaguzi na Katiba badala kutumia njia ya Maandamano.
Akizungumza na waandishi wa Habari Katibu wa Vyama 13 visivyo na Uwakilishi Bungeni jijini Dar es Salaam Doyo Hassan Doyo amesema kuwa wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo hawafiki kumi akidi haitoshi vyama hivyo vimeshituka Chama hicho kuja na Agenda ya katiba mpya ambapo wabunge hao wana idadi ndogo bungeni hawawezi kutoa mstakabali wa muswada katiba hiyo ikiwa wapo wa chache.
"Chadema wabunge wakuchaguliwa hawafiki kumi tumesituka watuhawa kumua muswada wa katiba mpya bungeni" Alisema Katibu Doyo Hassan Doyo.
Doyo Hassan Doyo alisema kuwa umoja huo unahitaji tume huru ya uchaguzi,Sheria vyama vya siasa dhamira yao nikuona nchi inakuwa ya Amani na utulivu.
"Dhamira yetu nikulinda Amani na utulivu wa nchi"Aliongeza Katibu wa vyama 13 visivyo na uwakilishi bungeni Doyo Hassan Doyo.
Katibu Mkuu wa Chama cha UDP Saum Rashid amesema kuwa Dhana ya Uongozi sio kutunishana misuli bali nikutumia Hekima na Maarifa kiongozi wetu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ametumia Hekima na maarifa .
Alisema ilikufikia Agenda 50/50 ya Usawa wa kijinsia kwa wanawake sisi wanawake mambo tuliyoyadai yametekelezwa anaye pinga mswada huu ni Adui yetu.
"Wanawake wengi hawapendi vurugu,tujifunze kutumia meza ya mazungumzo suala hili la maandamano hatuliafiki" Alisema Katibu Mkuu wa UDP Saum Rashidi
Aidha ,kwa Upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa vyama vya Siasa Visivyo na uwakilishi Bungeni Abdul Mluya ambaye ni Katibu Mkuu wa chama cha Demokratic Part (DP) amesema kuwa hali ya Siasa katika kipindi cha 2023/24 Kuwa Mwenyekiti wa Chama chadema Freeman Mbowe alipinga mswadwa wa Tume huru ya uchaguzi na kudai mwenyekiti huyo ataitisha Maandamano sisi hatukubaliani na kauli yake.
Alisema Vyama 13 visivyo na uwakilishi bungeni havikubaliani na uamuzi huo wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
"Uamuzi wa Chadema una viashiria vyote vya uvunjifu wa Amani Demokrasia ni majadiliano na katika majaadiliano kuna wanao yakubali na wasiyokubaliana"Alisema Mwenyekiti AbdulMdoya.
Mdoya alisema kuwa Muktadha wa kutokubaliana na Maandamano hayo nikutokana na kuwepo kundi la wazee,wajawazito,walemavu ambapo kunapotokea vurugu kundi hilo ndilo linalo athirika zaidi.
"mambo yaliyopendekezwa ni pamoja Muundo wa Tume ya uchaguzi,Maboresho ya sheria ya uchaguzi ,kuondolewa kwa mgombea bila uchaguzi Asilimia 60 yamaoni kwenye kikosikazi yamechukuliwa"AliongezaMwenyekiti wa vyama vya siasa visivyo nauwakilishi Bungeni Abdul Mdoya.
Post a Comment