Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Maji sambamba na kongamano la tatu la Kimataifa la Kisayansi la Maji ambalo limeandaliwa lililoandaliwa na Chuo cha Maji ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau mbalimbali ambao wameshiriki katika maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Maji sambamba na kongamano la tatu la Kimataifa la Kisayansi la Maji ambalo limeandaliwa lililoandaliwa na Chuo cha Maji
......................
NA MUSSA KHALID
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewataka viongozi wa Chuo cha Maji kuendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia ili kusaidia kutoa wahitimu waliobora katika tasnia ya sekta ya Maji watakaoweza kujiajiri/kuajiriwa na kuchangiza uchumi wa nchi..
Pia Dkt Kikwete amesema kuwa hatua ya serikali ya awamu ya sita Kuendelea kutoa fedha katika sekta maji imesaidia kuwezesha wizara ya maji kutekeleza miradi mbalimbali ya maji ambayo imechangia kuondoa changamoto ya upatikani wa maji safi na salama nchini.
Hayo ameyaeleza Jijini Dar Es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Maji sambamba na kongamano la tatu la Kimataifa la Kisayansi la Maji ambalo limeandaliwa lililoandaliwa na Chuo cha Maji na kukutanisha Wataalam mbalimbali wa sekta ya maji kutoka ndani na nje ya nchi,
Dkt Kikwete amesema Rais Samia Suluhu Hassan anaiishi kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani kwani maeneo mengi kwa Sasa nchini yameunganishwa na huduma ya maji safi na salama,
Naye Naibu katibu Mkuu Wizara ya maji Mhandisi Mwajuma Waziri amebainisha kuwa kongamano Hilo ni muhimu kwani litatoa fursa kwa wanazuoni na wataalam wengine kuweza kubadilishana Mawazo ya kuboresha na kuimarisha sekta ya maji nchini kupitia uchangiaji wa mada mbalimbali ambazo zitatolewa.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Maji Dkt Adam Karia amesema chuo kinapoadhimisha miaka 50 kimekuwa ni msaada mkubwa kwa serikali hasa katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ya maji kutokana na wahitimu wake kubobea katika sekta hiyo muhimu,
Maadhimisho ya miaka 50 ya chuo cha Maji na kongamano la tatu la Kimataifa la Kisayansi la Maji yamehudhuriwa na washiriki mia tano kutoka ndani na nje ya Nchi ambapo washiriki 48 watawasilisha tafiti zao ambazo zina mchango mkubwa katika sekta ya Maji
Post a Comment