MGANGA ALIYELEWESHA WATU 16 WA FAMILIA MOJA AKAMATWA

..............,....

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata na kumuhoji kwa kina mtu aliyejifanya mganga wa jadi Lucas Salumu Baswege (42)mkazi wa Kisemvule, Mkuranga kwa tuhuma za kuwanywesha dawa watu zaidi ya 16 maeneo tofauti tofauti dawa inayodhaniwa kuwa ni sumu na kuwaibia .

Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari jijini Dar es salaam Kamanda wa Jeshi Hilo (SACP) Muliro Muliro amesema kuwa  Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo alifanya matukio kama hayo maeneo ya MjimwemaKigamboni, Tuangoma , Kilungule, na Ubungo Dar es Salaam.

Amesema kuwa  Vitu vilivyoibwa  na mtuhumiwa huyo tayari vimekamatwa na Polisi ikiwemo pikipiki namba MC. 474 DUR aina ya boxeriliyoibwa Tuangoma,simu za mkoni 10ambazo tayari zimetambuliwa na wenyenazo.

Pia Jeshi hilo limemkamata Thomas Mhagama (35)Fundi simu wa Temeke Sandali ambaye amekuwa akishirikiana na mganga huyo wa jadi kwa kupokea simu za wizi na kuziuza kwa watu.

Kamanda Muliro amesema kuwa Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Katika hatua nyingine, Jeshi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2024 limemkamata Mariam Fransisco Renatus (22) kwa tuhuma za kumuiba mtoto wa (Miezi 10) 

Miracle Ayoubeneo la Gongo la Mboto, Dar es Salaam na kwenda nae hadi Geita, kijiji cha Bugalama.

Amesema  kuwa Jeshi la Polisi lilipokea taarifa za kuibwa kwa mtoto huyo tarehe 06 Februari, 2024 majira ya saa moja usiku kutoka wa mama wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Victoria Charles (34) Mkazi wa Gongo la Mboto.

Mwizi huyo alijifanya msaidizi wa kazi na baadae kupata fursa ya kumuiba mtoto huyo.

Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa mtuhumiwa alimuiba mtoto huyo kwa lengo la kuwaridhisha familia ya wakwe zake baada ya kuwadanganya kuwa alijifungua mtoto tangu mwezi wa Mei, 2023 baada ya kuwa na mahusiano na kijana wao.

Mtoto amepatikana akiwa na afya njema na mtuhumiwa atafikisha haraka iwezekanavyo mahakamani ili kijibu tuhuma zinazo mkabili.

Jeshi la Polisi linatoa wito kuwa makini na makundi ya watu wanaojitokeza kuwa ni waganga wa jadi na vijana wa kike wanaojifanya wanatafuta kazi za ndani na baadae kuweza kuwaibia. 


0/Post a Comment/Comments