MKOSOAJI WA PUTIN AFIA GEREZANI


                                **********

Mpinzani na mkosoaji mkubwa wa Rais wa Urusi Vladmir Putin, Alexei Navalny mwenye (47) amefariki dunia jana asubuhi katika gereza moja nchini humo.

Idara ya Magereza ya Urusi ilisema Navalny alijihisi mgonjwa baada ya matembezi asubuhi ya Ijumaa (Februari 16) na kupoteza fahamu.

Idara hiyo iliongeza kuwa juhudi za kumpatia matibabu ya dharura hazikufanikiwa na akafariki dunia.

Navalny alikuwa akitumikia kifungo cha zaidi ya miaka 30. Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov, alisema Rais Vladimir Putin tayari alikuwa amejulishwa kuhusu kifo hicho na kwamba ni jukumu la madaktari kufafanua sababu yake. 

#Dwkiswahili

0/Post a Comment/Comments