SERIKALI : TUTAHAKISHA AJIRA ZA WATANZANIA ZINALINDWA.

..................

Timothy Marko.

SERIKALI imesema kuwa katika kuhakikisha Ajira za watazania zinalindwa,Serikali imekubaliana na sekta Binafsi Ajira za watalamu wa Sekta ya Ununuzi, na Afisa Ununuzi kuwezakuajiri Watalamu wa kutoka nje.

Akihitimisha Kongamano la Uwekezaji na kodi  la mwaka  jijini Dar es Salaam  Waziri wa Uwekezaji Profesa  Kitlya Mkumbo amesema kuwa katika mapendekezo ya kongamano hilo lakikodi na uwekezaji lililo jumuisha sekta binfsi na Serikali  wameazimia kuwa serikali itaboresha mazingira mazuri ya kibiashara ikiwemo kuondoa vikwazo vya ufanyaji biashara na uwekezaji  nchini.

" Tumeazimia kuuboresha Mazingira wezeshi yatakayo wezesha Sekta binafsi na Ile ya Umma katika kukuza Uchumi"Alisema Waziri wa Uwekezaji Profesa kitlya Mkumbo.

Profesa Mkumbo alisema kuwa Nivyema Watalamu wakazingatia maadhimo ya kikao hicho cha siku mbili kilichofanyika jijini Dar es salaam ilikiweze kuleta tija katika Uchumi wa nchi.

Alisema lengo nikuhakikisha watanzania wanapata Ajira kupitia sekta ya Biashara .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanzania Comercial Benki (TCB) Adam Mihayo amesema kuwa sekta ya kibenki hupeleka fedha kwenye Maeneo yanayo chochea Maendeleo.

Alisema kuwaBenki hiyo imelenga  kuwapa Mikopo kwa wa wafanyabiashara wadogo takribani shilingi bilioni 300.

"Fedha hizi tumelenga kuwekeza katika Miundombinu na katika sekta ya Afya"Alisema Mkurugenzi wa Benki TCB Adam Mihayo.

Aidha ,Mkurugenzi Mkuu wa Benki wa Benki ya Biashara ya CRDB Majid Nsekela amesema kuwa sekta ya fedha ni kiunganishi  cha uchumi ambapo amebainisha sekta hiyo haiwezi kufanya vizuri Endapo  sekta ya Biashara haitofanya vizuri.

Alisema ni Vyema Serikali ikajikita kuangalia ni sekta Zipi za kimkakati ili ziendelezwe ilikuchochea Ukuaji wa Uchumi.

"Sekta ya kibenki  kazi yake nikukuchochea upatikanaji wa mitaji ili kuwezesha Ukuaji wa Biashara"Alisema Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Majid Nsekela.

Aidha Majid Nsekela aliomba Serikali kuweka Mazingira rafiki ya kodi ilikuchochea Ukuaji wa Biashara.

"Mnyororo wa thamani Uangaliwe sambamba uboreshaji wa mifumo ya kikodi"Alisema Majid Nsekela.

 

0/Post a Comment/Comments