SERIKALI: UPUNGUFU WA DOLA KUNATOKANA MIRADI YA MAENDELEO.


                                  *********

Timothy Marko

SERIKALI imesema hali ya Upungufu  wa Dola nchini ,imetokana na fedha nyingi zimetumika kugharamia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na kimkakati nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Fedha Dk.Mwigulu Nchemba amesema kuwa tatizo la kuadimika kwa fedha hiyo nitatizo la Dunia nasio Tanzania peke yake.

"Dola nitatizo la Dunia lakini kwa  upande wetu Tanzania tunayo Miradi Mikubwa tunatekeleza ambapo Gharama kubwa za Mradi zinatumia Dola nasio

 Fedha za kitanzania ili kutekeleza Miradi hiyo"Alisema Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba.

Dk .Nchemba alisema kuwa katika kuelekea Dira ya Maendeleo ya taifa 2050 imelenga kukuza Uchumi Jumuishi ambao una lenga kukuza sekta yakilimo ,Uvuvi ,na Mifugo.

"Hatakama kunamisukomisuko ya kiuchumi Duniani,Nchi yetu imekuwa na uchumi mzuri wadau wamaendeleo wametupongeza  kwakuwa na Mazingira  ya Uwekezaji"Alisema waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba.

Aidha ,Muwakilishi wa Wadau Wamaendeleo nchini ambaye ni Balozi wa Uingereza nchini David Conker amesema kuwa Sekta Binafsi ni kichocheo kizuri  cha Uchumi.

Alisema Wadau wa Maendeleo wapo tayari kuendelea kuchangia dira ya Maendeleo2050hasa sekta ya kilimo.

"inakadiriwa watu Milioni saba katika nchi ya Tanzania wapo chini ya Mstari wa kiwango cha Umasikini"Alisema Balozi wa Uingereza David Conker.

Balozi Conker alisema Wadau  wa Maendeleo wamelenga kukuza ushirikiana na Tanzania katika kuboresha Mazingira ya uwekezaji na Biashara nchini.

Alisema ilikuweza kuondokana na tatizo la Umasikini nivyema Rasmali watu wakakajengewa uwezo.

"Nivyema Tanzania ikaendelea kujikita katika sera ya Diplomasia ya uchumi ilikuweza kuchochea Uwekezaji na Biashara"Alisisitiza David Conker.

Kwaupande wake Mkurugenzi wa Taasisi yauchumi na jamii (ESRF) Profesa Fortunatus Makene amesema kuwa nivyema serikali ikatilia mkazo katika kuboresha sekta ya Elimu ikiwemo kurekebisha sera itakayochochea hali ya Ubunifu kwa Wahitimu.

Alisema ni vyema Eneo la kilimo biashara likatiliwa mkazo ilikuongeza ajira na kuchochea uchumi.

"Eneo muhimu nieneo la wafanyabiashara wadogowawadogo(SME) na wakati  wawezeshwe katika kuchangia uchumi"Alisema Profesa Fortunatus Makene.


0/Post a Comment/Comments