SERIKALI YADHAMIRIA KUKUZA SEKTA YA UWEKEZAJI.

 



                                

                                **********

Timothy Marko.

SERIKALI imesema itaendelea kukuza uwekezaji katika sekta za kimkakati ili kuchochea ukuwaji wa uchumi nchini.

Akizungumza katika kongamano la mwaka la kikodi na uwekezaji nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaa wa Makamo wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk.Philip Mpango amesema Moja ya mikakati ya serikali ya Awamu ya Sita nikukuza  Uwekezaji katika sekta ya uvuvi wa bahari kuu  pamoja na Sekta ya Madini ili kuweza kuongeza na kukuza pato la taifa.

"Upatikanaji wa takwimu sahihi na kuboresha Mazingira ya uwekezaji na  uzalishaji wa Bidhaa zenye ubora nikichocheo cha ukuaji wa uchumi" Alisema Makamu wa Rais DK Philip Mpango.

Makamu wa Rais Dk.Mpango alisema kuwa hatua ya Maboresho katika mfumo wa kodi na huduma za pamoja za forodha na kuwepo kwa ofisi ya usuluhishi wa masuala ya kodi kunatoa wigo mpana wa Makusanyo  ya kodi.

Alisema kwa miaka ya hivi karibubuni Tanzania imekuwa kitovu cha ukuaji wa uchumi unaoenda kwa  kasi katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki huku ukuwajiwake ni Asilimia 5.2 ikiwa na miradi ya maendeleo 526 ambayo imeandikishwa.

"Yote haya yana chagizwa na Marekebisho ya sheria kodi na Marekebisho viwango vya ushuru wa bidhaa nakutoa misamaha yakodi kwenye  Zana za kilimo,na vifaa vya Magari"Aliongeza Makamu wa Rais Dk Mpango.

Waziri  wa Uwekezaji Profesa Kitilya Mkumbo amessma kuwa lengo la serikali nikuunganisha sekta ya Uwekezaji na kuboresha mufumo yakikodi ilikuweza kuchochea ukuwaji wa uchumi.

Alisema ili wawekezaji waje nchini mwako wanazingatia Amani na utulivu na Mazingira ya kisheria wezeshi ya ufanyaji Biashara na upatikanaji wa Soko la Bidhaa zitakazo zalishwa .

"Jumuhia ya Afrika Mashariki inasoko la bidhaa la watu milioni 400,Jana Tumeanza Uwekezaji  wa SGR wawekezaji  wamevutiwa nauwekezaji nchini"Alisema Waziri wa Uwekezaji Profesa kitlya Mkumbo.

Profesa kitilya aliongeza kuwa  uboreshaji wa sera ,mipangona kanuni ni nyenzo muhimu ya kuwavutia wawekezaji.

"Tumefanya maboresho Maeneo 665 kati ya hayo 419 yamelenga kuboresha mazingira ya uwekezaji"Alisisitiza Profesa Mkumbo.

Waziri wa Fedha DK Mwigulu Nchemba amesema moja yamambo yanayotiliwa mkazo katika serikali ya Awamu ya sita ya Rais Dk Samia Suluhu Hassani niukuzaji biashara naukuaji wa uchumi.

Alisema ,hata hivyo serikali ya Awamu yasita imekuwa ikikabiliwa nachangamoto ya wigo mdogo wanaolipa kodi nakudhofisha juhudi za serikali.

"Jambo la ulipajikodi  ni jambo la Nchi na sio la TRA,TRA inakamilisha mifumo ya kodi naushuru wa forodha"Alisema Dk Mwigulu Nchemba.

.


0/Post a Comment/Comments