Na Magrethy Katengu
Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu imesema inakwenda kuweka Mkakati Madhubuti ikiwemo kufanya mapitio ya sheria na kanuni itakayokwenda kusaidia kudhibiti Ukatili wa watoto Mtandaoni.
Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam Waziri Wa Maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na Makundi Maalumu Dkt Dorothy Gwajima wakati akifungua Semina ya Usalama wa Mtoto Mitandaoni kwa Wahariri na Waandishi wa vyombo vya habari ambapo amesema Wazazi , Teknolojia inakwenda kwa kasi na na maudhui yanayosambaa mtandaoni ni hatari kwa watoto hivyo Elimu haina budi kutolewa kwa walezi kwani wamejisahau na kuwapa watoto hao vifaa vya kielektroniki ikiwemo simu Tv pasipo kuwa karibu nao kujua nini wanakitazama watoto
Waziri Dkt Gwajima amesema sambamba na hayo utaafiti uliyofanywa mwaka 2022 kwa watoto Tanzania unaonyesha umri wa miaka 12 hadi 17 ilibainika asilimia 67 ya watoto wanaotumia mitandao maarufu ikiwa ni pamoja na Facebook, Twitter (X), Instagram, Whatsap, Tiktok na Telegram na asilimia 4 ya watoto waliotumia mitandao walifanyiwa aina tofauti za
ukatili kwenye mitandao na wahalifu mtandaoni waliwasiliana huku asilimia 5 ya walishawishiwa au kulazimishwa kwa vitisho kutuma picha zao za utupu hivyo uangalifu unahitajika kwani licha faida nyingi za mitandaoni, athari zinazowakuta ni kutokana na kukosa uangalizi wa karibu.
Sanjari na hayo athari zinazotokea ambapo mlezi anakuwa hajui anashtuka mtoto kashaharibikiwa ikiwemo kuanza ngono katika umri mdogo hivyo kupata tatizo la kisaikolojia na mmonyoko wa maadili hii imechangia kuwepo vitendo vingi vya ukatili watoto kwa watoto kutokana na kuiga mtandaoni ikiwemo mwingiliano wa mila na desturi za mataifa mengine kuiga ushoga na usagaji.
"Tunakwenda kutoa muarobaini kuweka mikakati na za kisera na kisheria za Kimataifa, Kikanda na Kitaifa katika kuwalinda watoto na Vijana wa Balehe dhidi ya ukatili wa Mitandaoni zikiwemo Sheria ya Makosa ya Kujamiiana Na. 4 ya 1998 kifungu cha 12, Aidha, Vifungu vya 12 na 13 vya Kanuni za Maudhui mitandaoni, 2018 chini ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya
2010, Kifungu cha 13 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao, ya 2015 na Vifungu
vya 83 na 158 (1) na (b) vya Sheria ya Mtoto Na.21, 2009" amesema Waziri
Wazazi na Walezi tatizo tutasaidia na vyombo vya habari kutoa elimu ya uelewa kuhusu Ukatili wa Mtoto mtandaoni namna ya kujilinda pia tutafanya mapitio ya sheria na kanuni na kusogea kwenye teknolojia ili mtoto anapotumia vifaa vya teknolojia anakuwa salama hadhuriki na chochote ili tutengeneze kizazi kilicho bora na salama kinachotegemewa miaka ya usoni" amesema Waziri
Sambamba na hayo amesisitiza kuwa lazima Maudhui yasiyofaa yasimfikie mtoto kwani Wazazi na Walezi lazima wawe kipaumbele kutimiza wajibu wa kuwa karibu na vifaa vya kiektroniki kwa watoto wao wanavyovitumia kwa kuwaawekea muda maalumu kutumia vifaa kwani wengine hawalali wanakesha wakichati usiku kucha.
Kwa upande wake Yusuphu Kileo Mtaalamu wa Masuala ya Mtandao na Uchunguzi wa makosa ya kidigitali amesema Dunia ilivyo sasa mtoto mdogo wa miaka anaweza kuiwasha simu akatafuta kile anachokihitaji ikiwemo katuni hivyo baadhi ya nchi ilipogundua hilo zimeanza kuchukua hatua na Tanzania haijabaki nyuma mikakati inaanza mapema kwa kuanza na kuongezewa nguvu Sheria na taratibu kwani haizuiwi mtoto kutumia teknolojia lakini lazima Elimu itolewe kwanza matumizi sahihi ya mitandao
Sanjari na hayo amesema kumekuwa na tabia ya Wazazi kuwapa watoto simu pasipo kujua nini wanachokizatama mtandaoni hivyo amesema kabla ya Mtoto kupatiwa simu apatiwe elimu kwani wengine hutumia kutuma.picha na kuandika jumbe pasipo kujua kesho yake inaweza kuwaathiri hivyo sasa Wazazi walezi tambueni kuwa teknolojia ni nzuri lakini je wako anachokitazama kinaendana na yeye .
" Mzazi Mlezi hakikisha Usimwachie Mtoto wako kifaa cha kielektroniki kama hujui nini anachokitazama bora umnyang'anye kwani utakuwa unamsaidia sana atasoma vizuri hadi pale atakapopata kabla ya kumpatia simu mpatie elimu kwanza na kuwa karibu naye anachokitazama kwani kuna wengine walikurupuka na sasa wanajutia kuko
Aidha Februari 10 inatarajiwa kuafanyika tukio kubwa Dodoma la Uzinduzi wa kampeni usalama wa Mtoto Mtandaoni na uzinduzi wa Kamati ya
Ushauri ya Taifa ya Usalama wa Watoto Mtandaoni itakakayoongoza kampeni kauli mbiu ni “Usalama wa Mtoto Mtandaoni ni Jukumu letu Chukua hatua".
Post a Comment