**********
Timothy Marko
Katika kuhakikisha sekta ya Mawasiliano inachangia Uchumi nchini,Tanzania na Burundi zimetiliana Saini yamakubaliano ya kukuza Sekta ya Mawasiliano baina nchi hizo.
Mkataba huo wa Mawasilano wenye thamamani Shilingi Bilioni 3.3 unalenga kuboresha sekta ya Mawasiliano sambamba na uboreshwaji wa Matumizi ya Mkongo wa taifa baina ya Nchi ya Tanzania na Burundi na Ukanda wa Afrika Mashariki (EAC) sambamba na Ukanda wa nchi zilizokusini mwa Afrika.
Akizungumza katika Hafla ya utiliaji Saini Makubaliano hayo jijini Dar es Salaam Waziri wa Habari Mawasiliano na Tenknolojia Nape Nauye amesema kuwa utiliaji sani kati ya Shirika la Mawasiliano la Burundi BBS na Shirika la Mawasiliano nchini (TTCL), Kutaongeza ushirikiano baina Tanzania na Burundi na kuongeza Soko jipya la kibiashara.
"Serikali ya Awamu ya sita imelenga kukuza Sekta ya Mawasilino kwa kuimarisha Huduma za Mkongo wa Taifa ilikuweza kukuza Uchumi wa kidigitali"asema WaziriNape
Waziri Nape amesema kuwa utiliaji saini wa makubaliano hayo unalenga kufungua milango ya uwekezaji kati ya Tanzania na Nchi jirani.
Amesema kuwa ni vyema wananchi wote wa ukanda wa Afrika kuweza kujiunga na mkongo ili kuweka Mazingira bora ya Mawasiliano.
"Tunatoa Wito wa nchi zote za Bara la Afrika kuweza kujiunga na Mkongo huu wataifa ili kuweza kufanya Mawasiliano kwa urahisi zaidi"ameeleza Waziri Nape
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu BBS wa kutoka nchini Burundi Jeremi Diomede amesema mkataba huo wa ushirikiano Baina ya Tanzania na Burundi unalengakukuza mifumo ya Mawasiliano katika Maeneo yaManyovu,kwa Tanzania na kabanga nakobelo kwa watu burundi.
Alisema BBS ni kampuni inalenga kukuza Bishara baina yanchi hizo.
Naye Mkurugenzi wa TTCL Peter Ulanga akizungumza wakati wa makubaliano hayo amesema tukio hilo linakuza mahusiano ya kidiplomasia kati Tanzania na Burundi.
Amesema Mahusiano ya nchi hizo imekuwa ni nyenzo muhimu ya mashirikiano ya kiuchumi.
"Wateja wetu mmeona nguvu kubwa ambayo imekuwa ikiwekezwa katika kuboresha shirika"amesema
Post a Comment