TFRA YAKUNJUA MAKUCHA KWA KAMPUNI YA YARA TANZANIA LTD.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania -TFRA Joel Laurent wakati akizungumza na wanahabari kuhusu  Operesheni mbalimbali kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa mbalimbali ukiwemo Tabora mnamo tar 29/1/2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya ruzuku Tanzania Luis Kasela akizungumza na wanahabari kuhusu  Operesheni mbalimbali ambazo TFRA kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa mbalimbali ukiwemo Tabora mnamo tar 29/1/2024.
Afisa Mahusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania –TFRA Matilda Kassnga akiwaeleza jambo wanahabari waliohudhuria katika Mkutano wa Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Joel Laurent akizungumza na kuhusu  Operesheni mbalimbali kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa mbalimbali ukiwemo Tabora mnamo tar 29/1/2024.
Baadhi ya wanahabari ambao wamehudhuria katika Mkutano wa Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania -TFRA Joel Laurent wakati akizungumza na kuhusu  Operesheni mbalimbali kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa mbalimbali ukiwemo Tabora mnamo tar 29/1/2024.

....................

NA MUSSA KHALID

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania -TFRA imefunga maghala ya Kampuni ya Yara Tanzania Ltd katika Mkoa wa Tabora baada ya kubaini ikifungasha Mbolea iliyokwisha muda wake kwenye vifungashio vipya vinavyoonesha ikiwa bado inafaa kutumika.

Imesema Mbolea hiyo Ilikuwa jumla ya mifuko 16,889 ya kilogramu 5 sawa na tani 90 yenye samani ya Shilingi Milioni Mia Mbili Ishirini na sita (226,000,000) ambapo ni kinyume na Sheria ya Mbolea namba 9 ya mwaka 2009.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa  TFRA Joel Laurent wakati akizungumza na wanahabari kuhusu  Operesheni mbalimbali kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa m alimbali ukiwemo Tabora mnamo tar 29/1/2024.

Aidha Mkurugenzi huyo amesema Mbolea iliyokwisha muda wake haipaswi kufungwa upya kurudishwa sokoni hivyo imesimamisha shughuli zote za Biashara za mbolea sambamba na ghala la kampuni hiyo Mkoani Mbeya.

"Katika muendelezo wa Operesheni hizo Mamlaka kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani Songwe imeweza kubaini udanganyifu unaofanywa na baadhi ya Wafanyabiashara wakishirikiana na wakulima Mkoani Songwe ambapo wakulima walijiandikisha kwa kutaja mashamba hewa na hivyo kuwauzia Mawakala wa Mbolea namba zao za utambulisho wa mkulima Ili kunufaika na Mbolea za ruzuku kinyume na utaratibu hivyo wote waliobainika walikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria"amesema Laurent

Katika Hatua nyingine Mkurugenzi Laurent ameeleza Hali ya upatikanaji wa Mbolea hadi kufika Disemba 31 mwaka jana Ilikuwa ni tani 797,871 sawa na asilimia 89 ya mahitaji ya Mbolea kwa mwaka 2023/2024 ambayo ni tani 848,884.

Pia amesema kuwa Mpaka Januari 31 mwaka huu kiasi cha Tano 447,603 kimeuzwa ndani ya nchi na kufanya kiasi kilichopo kwa sasa kuwa tani 414,227 sawa na asilimia 103 ya mahitaji ya tani 401,281 zinazohitajika Ili kukamilisha msimu hivyo mwenendo kuonyesha hakutakuwa na upungufu wa Mbolea. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya ruzuku Tanzania Luis Kasela amesema mfumo wa kidigitali katika usambazaj wa mbolea ya ruzuku umesaidia kudhibiti vitendo vya udanganyifu Kwa baadhi ya Wakulika na wafanyabiashara 

Hata hivyo Mamlaka hiyo imeendelea kutoa onyo kwa wafanyabiashara,wakulima na kwa mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kufanya udanganyifu kwenye Mpango wa serikali kwa kutoa Mbolea za ruzuku kuwa Hatua kali za kisheria zitachukilisa dhidi yao.

0/Post a Comment/Comments