TMA YAWATADHARISHA WAKULIMA.

..................

Timothy Marko

MAMLAKA ya hali ya Hewa nchini ( TMA) imewatadhalishai Wananchi ,kuhifadhi Chakula na kuimarisha Miundombinu ya kilimo ili kuweza kuondokana na Athari za Mvua za Masika zinazo tarajiwa kuanza Mwezi March hadi Mei Mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Dkt  Ladius Chang'a amesema Mvua hizo zinazotokana na Hali ya Joto Bahari katika Bahari ya Hindi zitaathiri mikoa ya Geita Mwanza pamoja na Singida na kusababisha mvua za Vuli katika mikoa hiyo.

"Mvua za Vuli katika Mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro zinatarajia kuanza Mwanzoni Mwa wiki ya nne ya Mwezi Febuary ,Matukio haya ya mvua yataambatana na Mvua kubwa"Alisema Ladius Changa'

Kaimu Changa' alisema Mvua hizo zitaambatana na Unyevu katika Ardhi na kuathiri sekta kilimo cha Nyanya na Viazi.

Pia alisema Mvua hizo zinaweza kuleta Magonjwa ya takayo athiri Mwani Baharini.

"Wakulima wazao la Mwani wanatakiwa kwenda kwenye sehemu zenye kina kirefu kuweza kuzalisha zao hili"Aliongeza Ladius Chang'a

Kwa Upande wake Mtalamu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Ramadhani Omari amesema kuwa Nyanda za kaskazini Mvua za msimu zilianza tangu Novemba Mwaka jana katika Mikoa ya Rukwa,Mbeya,songwe ambapo mvua hizo zotaendela Mwezi Febuary na kusababisha joto la wastani.

Alisema hali hiyo inatokana hali ya joto la wastani katika Bahari ya Antlatic.

"Hali hii pia inaweza kuleta Athari katika sekta ya Usafirishaji sambamba Athari katika sekta ya Anga wakati huohuo sekta ya Uchimbaji wa madini inaweza kuathiriwa na Maporomoko ya udongo"Alisema Ramadhani Omari.
 

0/Post a Comment/Comments