WAKULIMA WA PARACHICHI KILIMANJARO WAFUNDWA



********

Wakulima wa mazao ya migomba na Parachichi katika katika Tarafa ya Usangi, Mwanga mkoani Kilimanjaro. wamepatiwa mafunzo ya Kilimo cha Parachichi. Pamoja na kupatiwa mafunzo hayo washiriki hao zaidi ya 50 waligawiwa miche 300 ya parachichi na migomba. 

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na taasisi ya TAHA yana lengo la kuwajengea uwezo katika kufanya kilimo chenye tija pamoja na  kukabiliana ushindani wa biashara ya kilimo Wilayani humo.

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo mtaalam na mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka TAHA Abdon Joseph amesema, lengo la mafunzo hayo ni kujenga uelewa kwa wakulima juu ya namna bora ya kufanya kilimo chenye manufaa hususani katika zao la parachichi.

"Ili kupata mazao bora lazima kilimo kifuate hatua na taratibu na mkulima aweze kupata mazao bora na kipato, tumeeleza hatua kwa hatua kuanzia uandaaji wa mashamba, uchaguzi wa mbegu kulingana na mazingira, utunzaji wake na kuchanganya mazao pamoja na elimu ya ujasiriamali katika zao la parachichi." Amesema.

Kampuni iliyodhamini mafunzo hayo *Ombeni Logistics Company* wameahidi kushirikiana na wataalamu wa kilimo kuanzisha mashamba darasa ili kutoa fursa zaidi ya mafunzo na uzalishaji wa mbegu na kudhamini ziara za mafunzo kwa wannachi wenye nia ya kujifunza kilimo.
Taasisi nyingine zikizoshiriki kutoa mafunzo ni pamoja na Maua Mazuri, East West Seeds na Agricentric.


 

0/Post a Comment/Comments