WANAOTUMIA HUDUMA YA INTERNET WAMEFIKIA MILL. 35-DKT MWASAGA

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama (ICTC), Dkt. Nkundwe Mwasaga akizungumza na wanahabari wa Kiss Fm ambao wamemtembelea Ofisini Kwake
.....,.........

NA MUSSA KHALID 

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama (ICTC), Dkt. Nkundwe Mwasaga amesema serikali inaendelea na mkakati wa kuelekea kwenye mapinduzi ya Kidigitali zaidi Ili kuzidi kuongeza ushindani na nchi nyingine katika masuala ya Teknolojia.

Dkt Mwasaga ameeleza hayo leo Ofisini kwake jijini Dar es salaam wakati akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja kwenye Kipindi cha KissRipoti kinachoruka kupitia kituo cha Radio Kiss Fm kujadlili upi mchango wa Tehama kwenye Maendeleo ya nchi katika Kipindi cha Miaka Mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Aidha Dkt Mwasaga amesema kuwa katika kipindi cha Miaka Mitatu ya Rais Dkt Samia wamehakikisha wanatekeleza Nguzo Tano za msingi ikiwemo kuangalia ujuzi katika masuala ya Tehama,ambayo kwa kiasi kikubwa imesaidia katika masuala ya uwekezaji.

"Pia tumewekeza kwa kiasi Kikubwa katika masuala ya Mtandao kwamba inakuwa salama na watu wanendelea kuitumia, tumekuza huduma za mawasiliano ambapo kuna minara zaidi ya 750 inajengwa tangu mwaka jana na nne inahusiana na uchumi wa Kidigitali yenyewe,mfano katika masuala ya kupeleka fyber kwa watu kazi ambayo inafanywa na makampuni mbalimbali ikiwemo TTCL"amesema Dkt Mwasaga

Amesema katika Miaka Mitatu ya Rais Samia watanzania wanaotumia huduma za internet wamefikia Mill 35 ikiwa ni namba kubwa katika matumia

Kuhusu Soko la intaneti Tanzania,amesema  linawavutia watu wengi kutoka katika mataifa mbalimbali ambao wanaomba vibali kuja kufanya shughuli zao hapa nchini.

Amesema kuwa kwa sasa Kuna program kubwa ya kiserikali kupitia Shirika la Posta wanatengeneza namna ya Biashara kutumika kimtandao

0/Post a Comment/Comments