ACT -WAZALENDO YAJITOA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR.

................

Timothy Marko.

CHAMA cha ACT wazalendo kimejitoa Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar kutokana kutoridhishwa na Umoja wa Serikali wa kitaifa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar Katibu Mkuu wa Chama hicho Ado Shaibu amesema imerdhia kufikia hatua hiyo kutokana kwa baadhi ya Viongozi wa Chama hicho kushikiliwa na Baadhi ya maofisa wa Serikali na kutoachiwa huru.

"Tunahitaji Mageuzi ya kimfumo katika Serikali ya Umoja wa kitaifa tumezika watu 24 kutokana machafuko ya Zanzibar,nakutokupata Muafaka wa jambo hilo"Alisema Katibu wa Chama cha ACT -wazalendo Ado shaibu.

Katibu Ado Shaibu amesema kuwa katika maadhimio ya Serikali ya Umoja wa kitaifa iliazimia kuwa kila chama kinayo haki ya kufanya Siasa inavyotaka.

Katika hatua nyingine Chama hicho kimefanya uteuzi wa Wajumbe Halimashauri kuu ambapo katika kutekeleza adhima yausawa wa kijinsia wa 50/50 katika utezi wa wajumbe 50 kimeteuwa wajumbe 24 ambao ni wanawake kushika hatamu ya Uongozi wa chama hicho.

Aidha Shaibu aliongeza kuwa katika uteuziwa ndani wa chama hicho umewateua wajumbe 15 katiyao tisa wanawake huku sita niwanaume .

"chama chetu cha ACT wazalendo, halimashauri ya Chama chetu kimewawateua wajumbe24 kati yao  tisa niwanawake na sita niwanaume"Alisisitiza Ado Shaibu.

0/Post a Comment/Comments