AKIBA COMMERCIAL BANKI YAWATAKIWA WAISLAMU WOTE MFUNGO MWEMA WA MWEZI MTUKUFU



...............

Na Mwandishi wetu

Akiba Commercial Bank (ACB) imewapongeza Waislam wote kwa kuwa Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani .

Pongezi hizo amezetoa Mkurugenzi Mtendaji wa ACB Bw Silvest Arumasi katika hafla ya futari iliyojumuisha Wateja , Wafanyakazi pamoja na Wadau mbalimbali wa benki hiyo ambapo ameshukuru kuitika na kutenga muda wao kujumuika pamoja nao hivyo kwao imekuwa ni faraja kubwa na heshima  kubwa sanaa.

"ACB imekuwa na utamaduni wa kufanya hafla ya kufuturisha kwa kila mwaka kwa ajili ya kuunga mkono ndugu zetu Waislam katika funga yao na pia ni njia nzuri ya kuboresha mahusiano ya benki na wateja wetu " amesema Mkurugenzi


Sambamba na hayo Akiba Commercial Bank inatambua na kuheshimu sana Imani za wateja, Wafanyakazi na wadau wake na kuupa umuhimu wa kipekee katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Hata  Bw. Silvest Arumasi amesema kuwa ACB inaendelea kuboresha na kupanua wigo wa huduma zake ili kuendana na soko kwa lengo ya kukidhi matarajio ya wateja, amewaomba wateja na umma kwa ujumla kuendelea kuiamini Benki hiyo ambayo imeweza kuwahudumia Watanzania wengi na kuleta maendeleo makubwa kwa wajasiriamali na Jamii nzima kwa ujumla.


Aidha  hafla hiyo iliyofanyika tarehe 25 Machi, 2024 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam fursa pekee kuwapongeza Waislamu wote kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, na amewashukuru wadau wote kwa kutenga muda wao na kujumuika pamoja katika Futari hiyo kwani kwa kitendo hicho kimeleta faraja na heshima kubwa sana.

0/Post a Comment/Comments