BOMOA BOMOA KUFANYIKA APRIL 12 MSIMBAZI







                             **********
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) umesema Aprili 12 mwaka huu utaanza zoezi la kubomoa nyumba katika Bonde la Msimbazi, Dar es Salaam ili kupisha ujenzi wa daraja

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam, Mratibu wa miradi ya Ushirikiano na benki ya Dunia Mhandisi Humprey Kanyenye, amesema kuwa awamu hiyo ya kutekelezaji wa zoezi Hilo itawahusisha wale ambao wamefikisha wiki Sita zilizotolewa baada ya kupokea malipo ya fidia hadi kufikia 29, Februari 2024. 

Aidha amesema kuwa waathirika 2,155 wameshalipwa kiasi Cha shilingi 52,612,072,623 kati ya 2,329 waliopo kwenye daftari la kwanza wameshakwisha pokea malipo yao.


Mhadisi Kanyenye alieleza kuwa kwa mujibu wa makubaliano ya utekelezaji wa zoezi hilo, waathirika wa mradi ambao wameshakwishapokea malipo yao wanatakiwa kuhamisha mali zao na kupisha eneo la mradi ndani ya wiki sita (6) baada ya kupokea fedha hizo kwenye akaunti zao.

“Waathrika wote wa mradi huu wanafahamu kuwa tuliwapa muda wa kuhama kwa makubaliano maalumu ya kimkataba yaliyowataka kuhama ndani ya wiki Sita (6) mara tu baada ya fedha kuingia katika akaunti zao, muda huo sasa umepita hivyo wanatakiwa kuondoka ili kupisha utekelezaji wa mradi,” alisema Mhandisi Kanyenye.

Alieleza pia kuwa walichelewa kuanza zoezi hilo kwa ajili ya kuwapa muda waathirika wa mradi kubomoa wenyewe kwa hiari ili kuokoa baadhi ya mali zao.

Aidha, alisema kwamba kati ya waathirika 2,329 waliopo kwenye orodha ya daftari la kwanza la ulipaji fidia, kufikia tarehe 21 Machi 2024, tayari waathirika 2,151 walikuwa wamelipwa kiasi cha shilingi bilioni 52.6

“Lakini pia kuna wale ambao hawakufikiwa katika uthamini wa awali kwa baadhi yao kugomea ama kutoonekana katika maeneo yao, idadi yao ni 466, hawa wameingizwa katika orodha ya daftari la pili ambalo limeshakamilika na litawasilishwa kwa Mthamini Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kusainiwa siku ya jumanne tarehe 26 Machi 2024 tayari kwa kulipwa fidia,” alisema Mhandisi Kanyeye.

Mradi unatekelezwa kwa muda wa miaka sita (6) (2022-2028) kwa gharama takribani shilingi bilioni 663 na lengo kuu la mradi ni kuimarisha ustahimilivu kwa kuweka mikakati ya kukabiliana na mafuriko na kuwa na matumizi bora ya ardhi katika eneo la chini la bonde la mto msimbazi ikiwa ni pamoja na kurudisha uoto wa asili katika uwanda wa juu wa bonde la mto msimbazi.

0/Post a Comment/Comments