COSTECH YAWAJENGEA UWEZO WADAU




....................

MOROGORO

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeendesha mafunzo kuhusiana na usambazaji wa matokeo ya utafiti kwa watafiti, wabunifu, watunga sera na wafanya maamuzi na wafugaji pamoja na kutengeneza vijarida sera viwili (2) kwa wadau wa mnyororo wa thamani wa sekta ndogo ya vyakula vya mifugo.

Mafunzo hayo na Kikaokazi hicho kinalenga kutoa ujumuishi na ushirikishwaji wa wadau muhimu wa Maendeleo ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na kusambaza matokeo ya utafiti kwa lengo la kutatua changamoto zinazo wakabili wananchi, tarehe 25 – 28 Machi 2024, ukumbi wa Ngorongoro – ulipo katika Shirika la Mzinga , kambi ya Magadu – Morogoro Mjini

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti, Wizara ya Kilimo na Uvuvi, Prof. Mohamed Sheikh ametoa rai kwa COSTECH kuendeleza juhudi za kuandaa wataalamu wa kusaidia watunga sera na watoa maamuzi waweze kutatua changamoto zinazoizunguka jamii yetu ili kunusuru upotevu wa rasilimali za nchi.

“COSTECH wana uwanja mpana kusaidia watunga sera na wafanya maamuzi kuweka mazingira mazuri. Vilevile Serikali kupitia Vyuo Vikuu pamoja na Taasisi za Utafiti na Maendeleo zikae pamoja kufanyia kazi mapendekezo yanayotokana na ushahidi wa kisayansi kwa kuzingatia matokeo ya utafiti kutoa sera zinazoweza kufanyiwa kazi ndani ya Serikali moja” alisisitiza Prof. Sheikh

Nae, Mkurugenzi Msaidizi wa Biashara za Ndani, Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hanifa Mohamed amesema ni muhimu kuboresha mnyororo wa thamani sekta ya mifugo ili kuimarisha upatikanaji wa bidhaa zitokanazo na mifugo pamoja na vyakula vya mifugo. Hali hiyo itasaidia upatakanaji wa malighafi za Viwanda na kupunguza utegemezi wa kutumia bidhaa toka nje.

Mafunzo haya maarufu kama ‘Knowledge Scaling project Fund’ yamefadhiliwa na Shirika la IDRC kupitia Taasisi ya Africa Centre for Technology Studies (ACTS). Vilevile – Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) iliwezesha ufadhili kiasi cha Fedha TZS 120,000,000/= utekelezaji ulioanza Machi 2021/21 na Septemba 2023/24 kwa mwaka huu wa Fedha.

Aidha, COSTECH inaendeleza kazi ya usambazaji wa matokeo ya utafiti kupitia uandaaji wa vijariba sera (policy briefy) tangu Disemba 2023, ili matokeo ya utafiti yatumike katika utengenezaji wa Sera rafiki na Upangaji wa Mipango ya Maendeleo inayozingatia msingi wa ushahidi wa kisanyansi (Evidence-based decision making). 

Tume inashirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ikiwani  utekelezaji wa Agizo la Serikali kupitia ongezeko la ubora na thamani ili kubiasharisha bidhaa za ndani kuuzwa nje ya nchi na kuvutia uwekezaji wa takribani asilimia 70 wa sekta ya mifugo na chakula nchini

0/Post a Comment/Comments