...........
Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha Sekta ya kilimo inaimarika Tanzania kwa kushirikiana Nchi ya italia imesema kuwa itaendelea kushikiana na Tanzania katika kukuza zao la palachichi nakuweza kutafuta Masoko la zao hilo.
Akizungumza nawaandishi wa Habari jijini Dar es salaam Balozi wa italia nchini Tanzania Riccardo Zucconi amesema kuwa katika kukuza Soko la zao la Palachichi nchini ,nchi yake imelenga kuwasaidia Wakulima wa zao hilo nchini kuweza kupata mbinu bora za uzalishaji wa zao hilo.
" Sambamba na kukuza zao la palachichi nchini,Nchi ya italia nimaarufu kwa kilimo cha ngano ,na zao la mchele "Alisema Balozi Riccardo Zucconi.
Balozi Riccardo aliongeza kuwa italia imekuwa mdau mkubwa katika kuboresha sekta yakilimo kwa kutoa zana kilimo ilikuwezesha nchi ya Tanzania kuweza kupata masoko ya bidhaa za kilimo .
Aliongeza kuwa italia imekuwa ikisafisha bidhaa zitokananazo na mazao yakilimo na mifugo ikiwemo viatu vya ngozi pamoja na bidhaa za mvinyo .
"Lengo letu nikuwasaidia wakulima wadogowadogo kuweza kupata masoko ya bidhaa zao nchini italia" Alisisitiza Balozi wa italia nchini TanzaniaRiccado Zucconi.

Post a Comment