JOKETI AWATAKA WANAWAKE KUGOMBEA UONGOZI.



.........

Timothy Marko

KATIBU Mkuu Umoja wanawake nchini (UWT) Joket Mwegelo amewataka Wanawake kukuza Ushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa zinazotarajia kufanyika Mwaka huu.
Akizungumza katika ofisi za Makao Makuu ya Umoja huo jijni Dar es Salaam Joket Mwegelo amesema kuwa nivyema wanawake wajumuhia hiyo na Chama cha Mapinduzi kuweza kujitokeza kugombea nafasi Mbalimbali katika Serikali za Mitaa.
"KATIKA Kuelekekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu ni wahamasisha Wanawake kugombea nafasi Mbalimbali za Uongozi kwa ngazi ya serikali za mitaa"Alisema Katibu UWT Joket Mwegelo.
Joket alisema kuwa katika ziara mbalimbali zilizofanywa na Mwenyekiti ya Jumuhia hiyo Mary Chatanda imeweza kuzinduliwa ikiwemo miradi ya Afya namaji.
Aliongeza kuwaMwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Dk Samia Suluhu Hassani amewataka wanawake kuweza kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi kwa Ngazi za Serikali za mitaa.
"Kama kuna mwanamke anania ya kugombea tumtie Moyo katika kugombea nafasi mbali mbali za Uongozi kwa ngazi ya serikali za mitaa 2024"Alisisitiza Joket Mwegelo.

0/Post a Comment/Comments