....................
Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha sekta ya Uwekezaji inaimarika Zaidi ya Makampuni 120yakutoka nchini China yanatarajiwa kuwekeza katika sekta ya Vipodozi,ambapo kati viwanda hivyo viwanda 60 vinatarajiwa kuwekeza katika sekta ya Nguo.
Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa Habari jijini Afisa Uwekezaji na Viwanda nchini Diana Mwamanga amesema kuwa katika kuhamasisha sekta ya viwanda na uwekezaji nchini Kituo cha Uwekezaji nchini(TIC) kinatarajia kuwaleta wawekezaji kutoka china ambapo zaidi ya makapuni 120 yakutoka china na Tanzania yanatatajiwa kushiriki katika kongamano la uwekezaji kimataifa March27 Mwaka huu katika Hoteli ya Johari Rotana.
"Kongamano hili litajumuisha sekta binafsina umma kati ya China na Tanzania,kongamano hili linalenga kuwakutanisha wabia mbalimbali wa sekta za madini,Nishati,na Viwanda"Alisema Afisa Uwekezaji Diana Mwamanga.
Afisa uwekezaji kutoka TIC Mwamanga alisemakuwa lengo la taasisi hiyo nikuweza kujenga na kuhamasisha Uwekezaji⁸ ilikukuza sekta yakilimo na viwanda.
Aidha,Muwakishi wa Makampuni yaliyohamasika kuwekeza nchini ,kutoka China Janson Huang amesema kuwa makampuni hayo yanatarajiwa kukuza ushirikiano kati China na Tanzania kuweza kucharijisha sekta za kiuchumi kwa kushirikiana Makampuni yakizawa pamoja nayale ya kutoka china.
"Takiribani Makampuni 60 ya kutoka China yanatarajiwa kuchagililisha uchumi wa Tanzania "AlisemaMwenyekiti wa Makampuni hayo, Janson Huang.
Post a Comment