KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda amemtaka Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Jerry Silaa kuwachukulia hatua Watendaji wa wizara hiyo waliobainika kudhurumu Haki za Wananchi katika sekta ya Ardhi wachukuliwe Hatua za kisheria.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa katika sehemu nyingi katika ziara yake kumekuwa utendaji wa wadhuluma kwa baadhi ya watendaji wa Serikali husan katika sekta ya Ardhi.
"katika ziara nimebaini uwepo wa malalamiko mengi ya wananchi juu ya kuwepo na kukithiri kwa vitendo vya utoaji wa Hati feki na Nyaraka za za Ardhi" Alisema Katibu Mwenezi wa CCM Paul Makonda.
Makonda alisema Ni vyema Waziri wa Ardhi Nyumba na Makaazi Jerry
Silaa kufanya Mapitio utendaji sekta hiyo nakuwachukulia hatua za
kisheria wanaodhulumu haki zawananchi.
Aliongeza kuwa kwa atayebainika mtendaji kudhurumu Mwananchi Ardhi wachukuliwe hatua za kisheria nawabainishwe.
"Ili kuondoa na kumaliza kabisa Migogoro ya Ardhi iliyokidhili nchini lazima Maeneo yote ya wazi yalindwe, Tumefikia hatua tuona mpaka watu wanakatwa mapanga na wengine kuchomewa Nyumba zao kwa sababu ya Migogoro ya Ardhi" Alisisitiza Makonda.
katika hatua nyingine makonda amewataka viongozi wa serikali
kutekeleza majukumu yao kwa mujibu ya ilani ya Chama cha Mapinduzi
2020/25 hususani ibara ya 160 imezungumzia Utawala bora nakuwataka watendaji
wote wa serikali wote nchini kuzingatia utawala bora.
Post a Comment