Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TMA),Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tanianchi (IPCC) Dkt Ladislaus Chang"a atoa ujumbe siku ya Hali ya Hewa Duniani ambayo hufanyika Kila tarehe 23 March kila mwaka.
Baadhi ya Matukio mbalimbali ya TMA KIA ikiendelea na mafunzo kwa wanafunzi wa Shule ya Secondary KIA katika kuadhimsha siku ya hali ya hewa duniani, 23/03/2024
.................
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amewataka Watanzania kuendelea kufutilia kwa karibu taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) kwa kua taarifa zinazotolewa mamlaka hiyo inatoa taarifa za huwakika ili kujikinga na Majanga.
Prof Mbarawa ameyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani ambayo hufanyika Kila tarehe 23 March kila mwaka.
Waziri Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) ndio imepewa mamlaka ya kutabili mwenendo wa hali ya hewa kila siku
Aidha Prof Mbarawa ametoa wito kwa Watanzania kufutilia utabairi unaotolewa na Mamlaka hiyo na kuchukua hatua ili kujikinga na Majanga
'Serikali inaendelea kuiwezesha TMA kununua vifaa vya kisasa ili utabiliwake uwe wa asilimia Mia moja'amesema Prof Marawa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TMA),Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tanianchi (IPCC) Dkt Ladislaus Chang"a amesema TMA inaendelea kuwa mstari wa mbele kutoa mchango katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi kwa kufanya tafiti na kuhamasisha matumizi ya sayansi.
Aidha amesema kuwa Huduma za hali ya hewa zinazotolewa nchini Tanzania zimeendelea kuwa bora zaidi katika historia ya nchi kabla na baada ya uhuru.
"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya uwekezaji mkubwa katika ununuzi na uboreshaji wa miundombinu ya uangazi sambamba na wafanyakazi kujengewa uwezo ambapo maboresho hayo ni pamoja na ufungaji wa vifaa vya kisasa vya kuhakiki utendaji kazi wa vifaa vya hali ya hewa rada za hali ya hewa, vifaa vya utambuzi wa matukio ya radi (Lightning detector) na kompyuta yenye uwezo mkubwa wa kuchakata data za hali ya hewa (Computer cluster)"amesema Dkt Chang'a
Amesema kuwa uwekezaji huo umeongeza kwa kiasi kikubwa ubora na usahihi wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa na tahadhari za mapema hadi kufikia wastani kati ya asilimia 80 hadi 98 juu ya asilimia 70 inayokubalika kimataifa.
Post a Comment