.......
Timothy Marko.
MWENYEKITI wa Taasisi Ongea na Mwanao Steve Nyerere ameowaonya wanaomkebei na kutoa maneno ya kashafa kwa kutumia Mitandao kwa kumkashifu Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na waandishi Habari jijini Dar es salaam Steve Nyerere amesemakuwa nivyema Vijana nivyema wakaa pamoja kumsemea Vizuri Rais Dk Samia Suluhu Hassan nakuwataka Jeshi la polisi kuchukua hatua kwa wale wanaomkebei na kutoa maneno ya kashfa juu ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan.
"Mnapoona Mama anatukanwa jitokezeni mjibuni ,Hawezekani kuna watu wanamtukana Mama watu wananyamaza kimya"Alisema Steve Nyerere.
Nyerere alisema kuwa nivyema wanasiasa wakamuacha Rais Dk Samia Suluhu Hassan aweze kumaliza awamu yake.
Alisema Rais Dk Samia anafamilia ya watu milioni 60,haitowezekana anajitokeza mtu mmoja au kikundi cha watu kina mkebei Rais Dk Samia Suluhu Hassan .
"Wanaharakati wanaotaka kufanya siasa wafanye Siasa za Ustarabu,isifike mahali mkafanya siasa za kupitiliza ni vyema mkaheshimu Haki za Binadamu haki za Binadamu zinaendana na tabia njema"Aliongeza Steve Nyerere.
Nyerere alisisitiza kuwa Nchi ya Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe kwa kulipa kodi.
Naye Mwenyekiti wa wasanii wenye Ulemavu Adora Michael amesema nivyema taasisi ya Ongea na mwanao ikawasaidiawatoto wenye Ulemavu kuweza kupata viatu.
Alisema kumekuwa na taabia kwa kikundi kinamchafua Mheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutumia mitandao yakijamii.
"Tuna muonya aache hiyo tabia ,Mama samia ni Mlezi amegusa kila sekta"Alisema Adora Michael.
Post a Comment