TAASISI YA ELIMU YA WAZIMA YAWATAKA WANANCHI KUJIENDELEZA KIELIMU.


                         *********

Timothy Marko

TAASISI ya Elimu ya Watu Wazima Nchini,imewataka Wananchi kuendelea kujiendeleza kielimu nakusisitiza Kuwa Hali yakujifinza na kukuza ujuzi haina Mwisho.

Akizungumza katika Ufunguzi wa kongamamo la Elimu bila Ukomo liloandaliwa na taasisi hiyo ,Mkurugenzi wa Tasisi ya Elimu ya Watu Wazima Profesa Michael Ng'umbi amesema kuwa Fasalfa ya Elimu bila Ukomo inalenga kuwa badilisha Watu waweze kujiendeleza kielimu kwani Binadamu awaye yoyote amezaliwa kujifunza na ataendelea kujifunza hadi Mwisho wa Uhai wake.

"Malengo ya Milenia ya 2030 yanawataka wananchi kuweza kujiendeleza kielimu pasipo kuwa naukomo wa Elimu"Alisema Profesa Michael Ng'umbi.

Profesa Ng'umbi alisema kuwa Kwakadri Dunia inavyoenda kasi kiteknolojia nivyema wananchi wajikite katika kukuza kiwango cha Elimu na ujuzi.

Alisema Nivyema Sera ya Elimu ikawajumuisha wale walionje kwenye mfumo wa Elimu kujiendeleza kielimu.

"Mtu moja anaweza kujifunza toka Anazaliwa hadi umauti yake na kujiendeleza kielimu"Aliongeza Profesa Ngumbi 

Profesa Ng'umbi alisisitiza Falsa fa ya Elimu bila kikomo kwa watu wazima inalenga wahitimu wa Elimu ya watu wazoma kuendana na kasi ya Mabadilko ya teknolojia.

0/Post a Comment/Comments