WACHIMBAJI WA MADINI WATAKIWA KUTUMIA MBINU BORA ZA KUDHIBITI VUMBI MIGODINI.




.,..........

Timothy Marko

WACHIMBAJI wa Madini wametakiwa kutumia njia bora za Uhifadhi mazingira katika Maeneo ya Uchimbaji wa madini ikiwemo kutumia njiabora za udhibiti wa Vumbi katika Maeneo ya Migodi.

Akizungumza katika Mkutano wa wadau wa sekta ya Madini (Tanzania Chamber of Mines) Msimamizi wa Masuala ya Madini kutoka kampuni ya Dua -A-Side ya Afrika kusini Masipa Fillipa amesema kuwa ni Muhimu kwa Makampuni yanayojihusisha na uchimbaji wa madini kuangalia njia bora za udhibiti wa Vumbi linalotokana na shughuli za uchimbaji wa Madini.
"Katika Kuangalia Shughuli za Uchimbaji wa madini tuna angazia nininamnagani tutapunguza madhara yatokanayo na Vumbi kwenye maeneo ya Migodi" Alisema Masipa Fillipa .

Mtalamu wa sekta ya Madini Masipa Fillipa alisema kuwa Vumbi katika Maeneo ya madini yana athari kubwa kwa Binadamu ikiwemo matatizo ya kifua .

Aliongeza kuwa Ulimwenguni Nchi ya Austaria imeweza kupunguza kiwango cha Vumbi katika migodi kwa Asilimia 60nakusisitiza kuwa shughuli za madini huchangia kusambaa kwa Ugonjwa wa Asthma.

"Shughuli za Kutumia Vilipuzi katika Migodi huchangia kuleta vumbi linaloleta Magonjwa ya kifua,Ninashauri wadau wa sekta ya Madini kutumia njia ya umwagilia maji katika maeneo ya uchimbaji ilikuweza kupunguza madhara ya Vumbi katika migodi"Alisisitiza Masipa Fillipa.

Fillipa alibainisha kuwa Asilimia 70 ya Vumbi katika maeneo ya Madini hutoka kwenye barabara zilizopo pembezoni mwa migodi.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Madini (Tanzania Chamber of Mine) Benjamini Mchwampaka amesema kuwa moja ya kazi ya taasisi hiyo nikushughulikia Masuala ya kimazingira migodini ikiwemo Usalama pamoja na Afya kwa wachimbaji madini migodini.

Alisema Sambamba na Masuala
hayo pia taasisi hiyo imejikita kuangazia mwenendo wa Usalama wa Mabwawa ya Maji migodini, Baadhi ya Mabwawa haya yana taka sumu ambayo nihatari kwa binadamu. 

"OSHA nimsimamizi wa shughuli zote za kiafya kwa wafanyakazi migodini"Alisema

 Benjamini Mchwampaka.
Mwenyekiti Mchwampaka aliongeza kuwa Osha ndio msimamizi mkuu wa shughuli za madini za kiusalama ambapo Mchimbaji anapimwa kabla na mara baada ya kuingia Migodini.

Naye,Mwenyekiti wa Chamber ya Madini ya Afrika Kazi Fransica Mushi amesema kuwa katika kongamano hilo wanaangazia juu ya kuwepo kwa teknolojia mpya ya kupunguza Vumbi katika maeneo ya madini.
Alisema kumekuwa na magonjwa yamlipuko katika maeneo ya Madini yanayotokana Vumbi.

0/Post a Comment/Comments