Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) amewaagiza
Mameneja wa Mikoa wa Wakala wa Barabara (TANROADS) kushirikiana na Wakala wa
Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) katika usimamizi wa Ujenzi na matengenezo
ya miundombinu ya barabara ikiwemo kushirikiana katika upimaji wa ubora na
viwango vya ukarabati wa barabara ya changarawe.
Bashungwa
ameeleza hayo leo tarehe 29 Machi 2024 baada ya kutembea kilometa 20 kwa miguu
Wakati akikagua Ujenzi wa Barabara ya Bweranyange - Kafunjo kwa Kiwango cha
Changarawe wilayani Karagwe Mkoani Kagera.
“Namuagiza Meneja wa TANROADS Mkoa Kagera
kushirikiana na Meneja wa TARURA Mkoa Kagera na Maneneja wote nchini
kushirikiana katika kuimarisha usimamizi wa maetengenezo ya barabara za
vijijini ambapo TARURA wanaitaji utalaamu kutoka TANROADS kwenye vipomo”
amesisitiza Bashungwa
Aidha, Waziri Bashungwa amemtaka Meneja wa TARURA
wilaya Karagwe kusimamia Wakandarasi wote wanaotekeleza matengenezo ya
barabara, kusimamia mashariti ya mikataba ikiwa ni pamoja na kushirikisha Madiwani
na Wananchi katika maeneo ambayo wanatekeleza miradi.
“Muwashirikishe Madiwani wa kata huska, wawe na BOQ
na wajue fedha iliyotolewa na Serikali katika eneo lake na kufahamu fedha hiyo
itajenga barabara yenye kiwango gani, karavati ngavi na mambo yote Mkandarasi
anayopaswa kuyatekeleza” amesema Bashungwa
Vile vile, Waziri Bashungwa amemshukuru Mheshimiwa
Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha fedha za ukarabari wa Kiwango cha
Changarawe Barabara za Bweranyange - Kafunjo km 20, Katojo - Ihembe - Rugu km
26, Kituntu - Rwakiro km 6 na Bweranganye Sekondari - Akagando km 6.
Kwa upande wake,
Meneja wa TARURA wilaya Karagwe Eng Kalimbula Malimi amesema matengenezo
ya barabara ya Bweranyange - Kafunjo km 20 kwa Kiwango cha Changarawe
utagharimu milioni 904.5 ambapo kazi ya
utekelezaji inaendelea.
Naye, Diwani wa Kata ya Nyabiyonza, Thomas Rwentabaza ameishukuru Seikali kwa kuwezesha matengenezo makubwa ya barabara hiyo ambayo ilikuwa haijawahi kutengewa fedha yoyote ambapo barabara hiyo itawezesha shughuli za maendeleo katika kata hiyo.



.jpeg)

Post a Comment