NA MUSSA KHALID
Hospitali ya CCBRT kwa kushirikiana na Taasisi ya utunzaji wa taarifa za mikopo Creditinfo zimeungana kwa ajili ya mpango wa kuchangisha msaada wa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano wenye ulemavu wa Ubongo
Pia kufuatia muunganiko huo watanzania wakiwemo watu wa sekta binafsi,makapuni binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali yameaswa kuunga mkono Juhudi katika kuleta mabadiliko kwa watoto wenye mitindio ya Ubongo waliochini ya uangalizi wa CCBRT ili waweze kusaidika.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Brenda Msangi ambapo amesema kwa mwaka huu Hospitali hiyo imeweka malengo ya kusaidia watoto 300 wenye mtindio wa ubongo nchini kwa kuwapa huduma ikiwa ni pamoja na ushauri na dawa tiba.
Aidha amesema kuwa mipango yao ni kuendelea kutoa huduma bingwa na bobezi hasa kwa wale watu wenye mahitaji kwa kuwatafuta wadau mbalimbali waweze kuwasaidia ili kuendeleza huduma hizo.
“Sisi kama CCBRT hizi huduma za utengamano wa watoto wenye utindio wa Ubongo kwa mwaka tunawapata kama 3000 wapya na wanaendeleao kupata matibabu endelevu kwa hiyo kwa mwaka tuna vipindi zaidi ya 9000 kwa ajili ya watoto hao’amesema Msangi
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utunzaji wa taarifa za mikopo Creditinfo Edwin Orasa amesema kuwa katika kusheherekea miaka 10 ya kuwa hapa Tanzania wameamua kutoa mchango wao kwa jamii ambapo imejitolea kukusanya Mill 100 ili kukabiliana na hitaji hilo.
‘Uamuzi wetu wa kuchangisha fedha kwa ajili ya CCBRT unatokana na rekodi bora ya hospitali ya kutoa huduma ya kina,hasa katika kushughulikia mahitaji ya watoto wenye ulemavu wa ubongo’amesema Orasa
Orasa amesema kuwa Creditinfo Tanzania itatoa asilimia 50% ya mapato kama mchango kwa watoto waliochini ya uangalizi wa CCBRT.
Nao baadhi ya wakina mama wanaowalea watoto hao wamesema changamoto ambayo wamekuw awakikumbana nayo ni kutoka kwa jamii kutokana na kuonyesha unyanyapaa kwa watoto wenye matatizo ya ulemavu.
Hata hivyo jamii imetakiwa kuungana kwa pamoja katika kusaidia watoto hao wadogo kustawi na kufikia uwezo wao kamili.







Post a Comment