DCEA YAKAMATA DAWA MPYA YA KULEVYA AINA YA ‘MDPV’

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam akitoa tathimini kuhusu operesheni waliyoifanya kwa ushirikiano na Vyombo vingine vya Ulinzi na usalama na TFS katika mikoa ya Shinyanga,Tabora,Iringa,Mbeya,Arusha na Dar es salaam.Baadhi ya Dawa za kulevya zilizokamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya katika operesheni waliyoifanya kwa ushirikiano na Vyombo vingine vya Ulinzi na usalama na TFS katika mikoa ya Shinyanga,Tabora,Iringa,Mbeya,Arusha na Dar es salaam.Madawa ya kulevya yakiteketezwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya

.................

NA MUSSA KHALID

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanikiwa kukamata Jumla ya Kilogram 54,506.553 za dawa za kulevya  mashambani na viwandani pamoja na kuteketeza ekari 262 za mashamba ya bangi katika mikoa mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo wakati akitoa tathimini kuhusu operesheni waliyoifanya kwa ushirikiano na Vyombo vingine vya Ulinzi na usalama na TFS katika mikoa ya Shinyanga,Tabora,Iringa,Mbeya,Arusha na Dar es salaam.

Kamishna Lyimo amezitaja Dawa zilizokamatwa kuwa ni bangi Kilo 54,589.65,mirungi Kilo 10.3,Heroin gramu 90.93,Cocain gramu 1.98 na Kilogram 4.623 za aina mpya ya Dawa za kulevya Methylene dioxy Pyrovalerone (MDPV) iliyokamatwa jijini Dar es salaam ikisafirishwa na raia wa Comoro aitwaye  Ahmed Bakar Abdou (32).

Aidha amesema kuwa watuhumiwa 72 wamekamatwa kuhusika na dawa hizo na baadhi yao tayari wamefikishwa mahakamani.

Kuhusu Dawa ya MDPV,Kamishna Lyimo amesema ni mpya ya kulevya iliyo katika kundi la vichangamshi inayotengenezwa kwa kutumia kemikali bashirifu na husababisha madhara ya haraka kwa mtumiaji ikilinganishwa na nyingine.

‘Dawa hii ya kulevya huuzwa kwa njia ya mtandao na husafirishwa kupitia kampuni za usafirishaji vifurushi na hufichwa kwa kuwekwa chapa za majina bandia kama bath salts,Ivory Wave,Plant Fertilizer,Vanilla Sky na Energy’amesema Kamishna Lyimo

Katika Hatua nyingine Mamlaka hiyo imebaini uwepo wa mashamba makubwa ya bangi katika hifadhi za misitu Ubangu mkoani Shinyanga na mabatini Mkoani Tabora ambapo wahalifu hao wamekata miti katikati ya misitu hiyo na kulima bangi.

Hata hivyo Kamishna huyo wameendelea kuwasisitiza wananchi kuonyesha ushirikianao kwa kutoa taarifa sahihi za wazalishaji na wauzaji wa dawa za kulevya katika maeneo yao ili kuweza kufanikisha operesheni mbalimbali wanazozifanya.

0/Post a Comment/Comments