Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El - Maamry
Mwamba,akizungumza wakati akifungua mkutano wa 37 wa Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha ambao umefanyika katika ukumbi wa Benki
Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.Baadhi ya Wajumbe wa mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha, wakifuatilia mawasilisho mbalimbali wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Meza kuu ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El Maamry Mwamba, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
...........................
NA MUSSA KHALID
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry
Mwamba,amewataka watumishi kufanya kazi kwa ushirikiano
kati ya idara na vitengo ndani ya wizara na taasisi kwa kuboresha mifumo ya
usimamizi wa fedha na mali za umma pamoja na kufanya ufuatiliaji na kaguzi za
mara kwa mara ili kujiridhisha na ubora wa miradi na thamani ya fedha
zinazotumika.
Dkt. Mwamba aetoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam
wakati akifungua mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha ambapo amewataka watumishi hao kuendelea kuzingatia misingi ya utawala
bora na sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ili kumuunga mkono Rais wa
Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuleta mageuzi
na mabadiliko ya kiuchumi nchini.
Dkt Natu amesema katika mkutano huo wafanyakazi
watapata muda wa kusikiliza mada mbalimbali na kuwataka kusikiliza kwa makini,
kujadiliana kwa uwazi na kufanyia kazi masuala yote muhimu yaliyoibuliwa katika
mkutano huo
Aidha,
Dkt. Mwamba amesema kuwa anatambua utendaji kazi na kuthamini mchango wa kila
mtumishi wa wizara na taasisi zake katika utekelezaji wa mipango ya Serikali na
kusisitiza kuendelea kuwajengea uwezo kupitia mafunzo ya muda mfupi na muda
mrefu ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na ubora unaostahili.
‘‘Ni lazima tutambue kuwa mikutano kama hii
inatupa fursa ya kuzungumza na kujadili masuala ya msingi ya utendaji kazi na
kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na wadau wetu. Inatupasa kutambua kuwa
Wizara ya Fedha ni taasisi muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu, hivyo hii ni
fursa ya kujadiliana masuala mbalimbali ili kuboresha utendaji wetu wa kazi’’,
alifafanua Dkt. Mwamba.
Awali akizungumza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Jenifa
Omolo,amesema kuwa kikao hicho kinafanyika kwa mujibu wa sheria ya ajira na
mahusiano kazini sura namba 336 kwa lengo la kuongeza ushirikishwaji wa
watumishi katika masuala mbalimbali ya Wizara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi
Wizara ya Fedha Bi. Scholastica Okudo, ametumia fursa
hiyo kusema kuwa watumishi wa Wizara ya Fedha wamejipanga kufanya kazi kwa
bidii na kwa weledi kuhakikisha kuwa maagizo yaliyotolewa na yatakayoendelea
kutolewa na viongozi yanafanyiwa kazi kwa ufanisi kwa ustawi wa Taifa kwa
ujumla.
Aidha
amesema kuwa watumishi wamejipanga kuhakikisha kuwa masuala yote ya kiutendaji
yanafanyika kwa kufuata Sheria kanuni na taratibu na pia kuhakikisha kuwa
wanazuia mianya ya rushwa inayoweza kujitokeza na Imani yao ni kuwa mifumo
iliyoweka na Serikali inasaidia katika kuzuia mianya ya rushwa.
Mkutano huo wa siku mbili umekutanisha wajumbe kutoka Wizara ya Fedha pamoja na taasisi zilizo chini yake kwa ajili ya kusikiliza mawasilisho mbalimbali, kujadili kwa uwazi pamoja na kufanyia kazi masuala yote muhimu yatakayo ibuliwa katika mada hizo na kuboresha utendaji kazi kwa maslahi mapana ya Taifa.

Post a Comment