JOKET AWATAKA VIJANA KUJENGA CHAMA,KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI





                             ********


Timothy Marko.

KATIBU wa Umoja wa Vijana wa  Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Joket Mwegelo, amewataka Vijana wa Chama cha Mapinduzi kuweza kukijenga chama.

Amesema Vijana wanapaswa kulinda kura na kugombea nafasi mbalimbali zinazo tolewa na chama hicho na Chaguzi nyinginezo ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarjia kuanza mwezi Oktoba Mwaka huu.

Akizungumza baada ya Siku moja ya kuteuliwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Dk.Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam, Mwegelo amesema kuwa Vijana wa chama hicho ndio uhai wa chama nakutanabanisha Vijana ni sawa na Damu katika Chama.

"Nina Mshukuru Sana Mwenyekiti wa Chama  Dk.Samia Suluhu Hassan  kwa kunipa heshimaya  kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana UVCCM na kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hii UVCCM"Alisema Mwegelo .

Katibu Mkuu UVCCM Joket alisema kuwa katika ngazi za Uongozi wa Chama hicho imempa historia kubwa kwa kipindi kifupi kuwa Mtendaji pekee wa UWT na UVCCM kwa vipindi tofauti tofauti.

Alisema kuwa tafiti zinabainisha  kuwa  Viongozi imara wanaoweza kuongoza nchi wanapatikana ndani ya Chama hicho.

 "Tunatambua nafasi za Vijana katika Chama ni walinzi wa kura ,Vijana inatupasa kushambulia kila kona  kuhakikisha Ushindi unapatikana katika chaguzi zijazo katika chama chetu"Alio geza Joket Mwegelo.

Naye Mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi wa Chama hicho UWT Ally Hapi, amesema kuwa lengo la jumuiya hiyo katika chama ni kuwalinda vijana ili chama hicho kuwa imara na bora.

Alisema kuwa Lengo la Jumuiya ya Wazazi ni kuakisi Sura ya Chama hicho kwa Wanachama wa chama hicho sambamba  Wananchi, Nchini.
"Tunayokazi ya kuleta Ushindi wa kishindo,Ogopa Sub za Dakika  za majeruhi " Aliongeza Ally Hapi.

Aidha,Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) CPA.Amos Makala amesema kuwa kuteuliwa katika nyadhifa hiyo nikama kurudi nyumbani  amempongeza Mwenyekiti wa Chama hicho kumteua kushika Wadhifa huo,nakusisitiza kuwa ataendelea kukijenga chama hicho kwenye ngazi ya Shina.

Alisema kume kuwa na Baadhi ya Watu kwenye Mitandao wakimkumbusha Wajibu wa nafasi hiyo aliyopewa na Mwenyekiti wa chama hicho nakubainisha kuwa atafanya kazi kwa Weledi nakuzingatia Misingi ya Chama hicho.

"ili tuweze kukamata Dola lazima tuanzie katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa hiyo haina shaka "aliongeza CPA Amosi Makala.

0/Post a Comment/Comments