MVUNGI AENDESHA KIKAO KAZI CHA WATAALAM WA REGROW

..............

Na Sixmund Begashe

Mkurugenzi wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Abdallah Mvungi leo Mkoani Morogoro ameongoza kikao kazi cha Wataalam kutoka Taasisi zinazotekeleza mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania REGROW kwa lengo la kufanya tathmini ya matokeo ya Mradi huo.

Katika kikao kazi hicho, Bw Mvungi amewapongeza watendaji hao kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kusimamia utekelezaji wa mradi hali inayopelekea wananchi kunufaika moja kwa moja huku Uhifadhi wa Maliasili ukiendelea kuhimarika pamoja na Shughuli za Utalii kutokana na maboresho makubwa ya miundombinu katika Hifadhi za kimkakati Kusini mwa Tanzania.

Mradi huo mkubwa nchini, ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwaletea wananchi maendeleo ambapo Maelfu ya Watanzania, wanaendelea kunufaika kwa ajira, elimu, Biashara za Jumuia na binafsi huku ukitarajiwa kuleta maendeleo makubwa zaidi ya maendeleo nchini pindi utakapo kamilika

0/Post a Comment/Comments