Dkt BITEKO KUFUNGUA KONGAMANO UWEZESHAJI KIUCHUMI APRIL 27.


.............

Na.Timothy Marko

NAIBU WAZIRI MKUU Dkt Dotto Biteko anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika kongamano la nne la Ushiriki wa watanzania kwenye Uchumi na Uwekezaji (local Content) April 27 hadi 28 Mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuuchumi Being' Issa amesema kuwa kongamamo hilo la Ushiriki wa watanzania kwenye Uchumi na uwekezaji linalenga kuwajengea uwezo wananchi kiuchumi ilikuweza kujikwamua kiuchumi nakuondokana na Umasikini wa kipato .

"Kongamano hili la nne linatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam tarehe April 27 hadi 28 ,Mgeni Rasmi anatarajiwa Kuwa Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Dotto Mashaka Bitteko"Alisema Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)Being Issa.

0/Post a Comment/Comments