TMA YAPONGEZWA KWA KUTOA TAARIFA ZENYE USAHIHI.

Afisa Kilimo Mkuu Manispaa ya Temeke na Mwenyekiti wa Chama cha wanawake Viongozi katika Kilimo na Mazingira (TAWLAE) Elde Saul Kimaro akizungumzia namna wanavyozitumia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania –TMA

.......................

NA MUSSA KHALID 

Wadau wa Masuala ya Kilimo nchini wamesema wataendelea kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania –TMA ili kupata taarifa za misimu mbalimbali ya mvua itakayosaidia waweze kuzalisha katika mashamba yao.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Afisa Kilimo Mkuu Manispaa ya Temeke na Mwenyekiti wa Chama cha wanawake Viongozi katika Kilimo na Mazingira (TAWLAE) Elde Saul Kimaro amesema kuwa ili mkulima aweze kuzalisha anahitaji maji na hasa ya mvua. 

Amesema kuwa taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa na TMA huwa wanazifikisha kwa maafisa ugani kwenye kata zao ili waweze kuzitoa kwa wakulima ili waweze kulima kwa kuzingatia misimu ya mvua. 

"Mamlaka ya Hali ya Hewa sisi Huwa tunashirikiana nao kwani taarifa zote wanazozitoa na sisi Huwa tunazifikosha kwa Maafisa ugani wetu kuhakikisha wanalima Kilimo kwa kuangalia Hali ya Hewa iliyopo Kwa wakati huo"amesema Bi Kimaro 

Amesema kuwa katika msimu huu wa masika ni muhimu wakulima wakahakikisha wanafuatilia taarifa sahihi  ili ziweze kuwasaidia kufanya kilimo sahihi kwa mazao yatakayowaletea tija. 

Amesema kutokana na TMA KWA sasa kutoa habari ambazo ni sahihi zinasairiq hata watulima kujua kuzitumia taarifa hizo katika Kilimo chao kama mvua zitakuwa nyingi au chache. 

Ikumbukwe kuwa Mwezi Februari mwaka huu wakati akitangaza mwelekeo wa msimu wa mvua za masika 2024, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya hali ya hewa, Dkt. Ladislaus Chang’a aliwahimiza wakulima Nchini kuandaa mashamba pamoja na kutumia teknolojia za kuzuia kutuama kwa maji hasa katika kipindi cha mvua za masika.

Katika hatua nyingine Kimaro  ameeleza changamoto ambazo wanakutana nazo kuwa ni pamoja wakulima kutokuwa na elimu ya umuhimu wa matumizi ya mbolea lakini pia uwepo wa bei kubwa ya pembejeo na kushamiri kwa wadudu.

 

Hata hivyo wakazi wa Dar es salaam wamehamasishwa kuendelea kufanya shughuli za kilimo na ufugaji kwani kina lipa na kinasaidia kila mtu kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kujipatia kipato.

0/Post a Comment/Comments