UBUNGO YAADHIMISHA MIAKA 60 YA MUUNGANO,YASITIZA KUENZIWA NA KULINDWA

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Hassan Mkwawa akizungumza na wanahabari baada ya ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano ambao umefanyika kwenye Ukumbi wa Noble Hall Kimara iliyopo katika wilaya hiyo.
Luteni Kanali mstaafu Ally Shamte akielezea historia ya Muungano katika kongamano la maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano ambao umefanyika kwenye Ukumbi wa Noble Hall Kimara iliyopo katika wilaya hiyo.
Afisa msemaji wa Taasisi ya Kizalendo Tanzania (TPO) Mkoa wa Dar es salaam Kanal Mstaafu Massanja Sunday akielezea thamani ya Muungano katika kongamano la maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano ambao umefanyika kwenye Ukumbi wa Noble Hall Kimara iliyopo katika wilaya hiyo.


Baadhi ya washiriki wa Kongamano Hilo wakizungumza na kutoa mitazamo ya kuhusu kuuenzi na kuutunza Muungano wetu kongamano la maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano ambao umefanyika kwenye Ukumbi wa Noble Hall Kimara iliyopo katika wilaya hiyo.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano Hilo wakisikiza kwa makini Maoni ya wadau mbalimbali kuhusu Muungano.
.....,.,.........

NA MUSSA KHALID 

Watanzania wametakiwa kuendelea kuuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiwemo kuulinda na kuuombea kwani umeleta mafanikio makubwa kwa Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Hassan Mkwawa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo wakati akifungua kongamano la maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano ambao umefanyika kwenye Ukumbi wa Noble Hall Kimara iliyopo katika wilaya hiyo.

Mkwawa amesema kuwa ni vyema wananchi wakauthamini muungano licha ya changamoto mbalimbali ambazo unapitia ikiwemo baadhi ya watu kutaka uvunjwe.

"Kutokana na waasisi wetu walivyosimamia Muungano huu ambao utakwenda kuadhikishwa April 26 ni Kila Mtanzania anapaswa kuuenzi na kuuliza ipasavyo"amesema Mkwawa

Kwa upande wake Luteni Kanali mstaafu Ally Shamte ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wazee na vijana kuwaenzi waasisi wa muungano kwani kwa busara zao ndio walioamua kuungana na kufanya nchi mmoja.

Amesema kuwa wazee wote waliokuwepi Kipindi cha Muungano unafanyika wanaelewa umuhimu wake ikiwemo katika kuleta Umoja na mshikamano.

Kwa upande wake Afisa msemaji wa Taasisi ya Kizalendo Tanzania (TPO) Mkoa wa Dar es salaam Kanal Mstaafu Massanja Sunday amewasisitiza watanzania kuendeleza yale waliotuachia waasisi wetu.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa Kongamano Hilo wamefarijika Manispaa hiyo kuandaa kongamano Hilo kwa linawakumbusha kuhusiana na historia ya namna mataifa hayo yalivyoungana kwa pamoja na kutengeneza nchi mmoja.

Maadhimisho hayo yamekwenda sambamba na kauli mbiu isemayo "Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tumeshikamana,na tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa letu"

0/Post a Comment/Comments