Na Mwandishi Wetu
Maduka ya Skechers yamewaletea viatu ambayo vimetengenezwa kwa teknolojia ya Hali ya juu (viatu tiba) ambayo havisababishi maumivu Wala malengelenge kwa watumiaji.
Akzungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Meneja masoko wa Skechers Tanzania, Micky Decha amesema kampuni hiyo imeamua kuja na viatu hivyo ili Kupunguza magonjwa ya miguu yanayotokana na viatu kwa watanzania.
Dkt Jamil Suleiman kutoka hospitali ya Tiba Healthcare amesema kwa muda mrefu kumekuwa na watu wanaogua maumivu ya mgongo na miguu ambao wengi huugua kutokana na viatu wanavyovaa.
Amesema kupitia viatu hivyo ambavyo vimeletwa na kampuni ya Skechers Hapa nchini vimewasaidia watanzania wengi ikiwemo wagonjwa ambao yeye amekuwa pia akiwatibu.
Viatu hivyo vina uwezo wa kuvaliwa kwa muda mrefu bila maumivu yoyote ya miguu kwani vimetengenezwa kwa viwango vya hali ya juu.
Post a Comment