..........
Na.Timothy Marko
BAADHI ya Madereva Bodaboda waliopo kandokando ya Ukumbi wa MwalimuNyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam Wameiomba Serikali kuwapa Vitambulisho Maalum ili kuweza kutambulika katika kazi zao.
Wakizungumza kwa Nyakati tofauti Bodaboda hao ,Moja wa6 dereva bodaboda kando kando ya Ukumbi wa kimataifa waMwalimu Nyerere uliopojijini Dar es salaam James Ngusi amesema kuwa wamekuwa wakipitia Changamoto ya kutotambuliwa na Serikali kama Ajira Rasmi nakufukuzwa kwenye maeneo wanayotoa huduma ya Usafiri hususan katika Viunga vya Ukumbi huo.
"Tumekuwa tukipata Shida katika kazi zetu tunaiomba Serikali itupe vitambulisho maalum kwani Boda Boda nikama kazi zingine"Alisema James Ngusi.
Naye James Mwita ambaye ni Dereva Mkabala mwa Ukumbi huo John Mwita amesema kuwa wamekuwa wakisumbuliwa kutokana kutopata Vitambulisho vya kazi zao na kuiomba Serikali kuweza kuwa tambua kama Ajira Rasmi inayo waingizia vipato kwenye familia zao.
kumekuwa na waendesha pikipiki wasiofanya kazi za Bodaboda Baadhi yao hujihusisha na vitendo vya kihalifu lakini sio wote.
"Mimi hapa Nimepata leseni ya Daraja A ya Udereva tunaiomba Serikali itupe Refleta maalum zitakazo tutambulisha"Alisema Dereva BodaBoda John Mwita.

Post a Comment