Mwandishi wetu.
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Brigedia Jenerali Hosea Ndagala amefanya ziara ya kutembelea Wilaya ya Kigamboni kata ya Mjimwema Mtaa wa Maweni kwa lengo la kuangalia madhara yaliyotokea kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam.
Awali akiwa katika kikao cha pamoja na Katibu Tawala Msaidizi (Mipango na Uratibu) Chillah Moses kuhusu madhara hayo ameelezwa kuwa jinsi ambavyo mvua hizo zimeleta athari katika maeneo mbalimbali ikiwemo kata ya mji mwema.
Maeneo mengine yalioathiriwa na mvua hizo katika wilaya ya Kigamboni ni pamoja na Maweni, biasi ambapo yamezingirwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha katika mkua huo.
Jenerali Ndagala ameelezwa hayo katika Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambapo serikali ya Mkoa huo umeendelea na jitihada mbalimbali ikiwemo kuyafikia maeneo yalioathiriwa na mvua hizo.
katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwaajili ya kupata taarifa kuhusu hali halisi ya madhara ya mvua hizo kwa Wilaya ya Kigamboni alielezwa kuwa maeneo yaliyoathiriwa ni pamoja na Mtaa wa Maweni eneo la Bondeni kata ya Mji Mwema pamoja na Maweni eneo la Biasi ambayo yamezingirwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo
Aidha Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu itaendelea kuratibu masuala ya menejimenti ya maafa nchini ili kuhakikisha jamii inaendelea kuwa salama na stahimilivu dhidi ya maafa.
Post a Comment