*************
Na Magrethy Katengu Dar es salaam
Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) leo wamefunga
mafunzo kutoka kwa wataalamu wa idara ya Tehama
ambayo yamejikita katika kadi janja zitakatumika katika mfumo wa nauli kabla ya abiria kuiingia kwenye geti anatumia kadi badala ya
kulipa nauli keshi.
Akizungumza leo Mei
17,2024 Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka Dart, Athumani Kihamia wakati wa kufunga mafunzo
hayo ya siku 5 kwa wahitimu 10 yaliolenga utunzaji wa usalama za kadi janja na
nywila zake kutoka kampuni ya Adva ID kutoka nchini India.
Hata hivyo Mkurugenzi amefafanua kuwa, hadi sasa mageti
zaidi ya 300 yaliyogharibu zaidi ya
bilion 11 na ujenzi wake umeshaanza na kufikia 67% itasidia kudhibiti mapato
kwa watumishi wasio waaminifu,.
"Kadi janja ni kadi zinazotumika katika mfumo wa nauli
lengo la Dart ni kufunga maeneo mengi
huku timu kubwa ya vijana mahiri ambao
tutakaa nao kwa miaka 10 ili iwe rahisi kupeana ujuzi na vijana wengine wapya
watakao ajiriwa, tunataka kuboresha mifumo yetu ili tutoe huduma zenye
ubora"amesema Kihamia.
Hata hivyo, amesema kuwa siku chache zijazo baada ya mwezi
wa 6 wataanza kutumia mageti hayo ambapo wameshaingiza mageti janja kutoka nje
zaidi ya 300, yatatumika katika mfumo wa nauli yataepusha katika uvujaji wa
nauli, mapato na watumishi wasio waaminifu, pamoja na kuokoa muda.
Naye Mkurugenzi wa teknolojia habari na mawasiliano Dart
Ng'wanashigi Gagaga amesema baada ya Mafunzo ya
kujenga uwezo wa timu ya
wanaoshughulikia mfumo wa nauli katika mageti yatakayotumia na kadi na
mpaka sasa kituo cha Korogwe kimeshakamilika na vingine vinaendele na
matengenezo.
"Ubora wa Mageti haya janja yatakayofungwa mfumo
maalumu na kuanza kutumika abiria
atakapofika na kadi yake itamwonyesha kiasi cha fedha kama hakitoshelezi
akaongeze hivyo hakutakiwa na matumizi yeyote ya karatasi tuko kidigital zaidi
" amesema Mkurugenzi Tehama .
Naye Muhitimu wa Mafunzo hayo Jackson Kazaura ameshukuru
kupata mafunzo hayo hivyo ameahidi ujuzi huo anakwenda kuutumia na kufundisha
wengine .
Naye Mwakilishi wa Wataalamu Kampuni waliyotoa mafunzo Kadi janja Advan IDe, Duncan Chege amesema
wanaamini mafunzo hayo waliyotoa wakufunzi
wataenda kutekeleza progaram hiyo kwa weledi zaidi huku wakiwafundisha
na wengine ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria .
Awali mafunzo hayo yaliwahi kutolewa mwaka 2000 lakini
kutokana na kuhamishwa hamishwa wakurugenzi hivyo yametolewa mwaka huu 2024 na
wataalamu hawa wataanza kuyafanyia kazi.
Aidha onyo kali limetolewa kwa madereva wanaoendesha magari ya serikali na
maboda boda na magari binafsi kuacha mara moja
kutumia njia ya mwendokasi bila kibali maalum kwani kufanya hivyo ni
kuvunja sheria na kusababisha ajali zisizo za lazima.





Post a Comment