IA KUONGEZA TIJA NA USHINDANI WA KIBIASHARA



**************

NA Mwandishi wetu

Imeelezwa kuwa  akili mnemba (IA), itasaidia kuongeza tija na ushindani wa Biashara huku elimu zaidi ikihitajika kwa wadau na wananchi kuhusu Teknolojia hiyo.

Kauli hiyo imetolewa  Jijini Dar es Salaam, na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), William Erio, katika kongamano la siku moja la kujadili matumizi ya akili mnemba yanayozingatia haki na uwajibikaji kwa mlaji.

Erio amesema kuwa hivi sasa Biashara nyingi zinafanywa kwa njia ya mifumo ya kimtandao na huduma nyingi zinatolewa na akili mnemba, hivyo FCC inaangalia jinsi ambavyo inaweza kutumia Teknolojia hiyo kumlinda mlaji kwa mujibu wa kanuni na Sheria

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya FCC, Dk Agrey Mlimuka amesema kuwa azma hiyo itakuwa na maana pale mifumo ya kiteknolojia itazingatia uwajibikaji ,tija, ,haki na usawa kwa kuwekewa mifumo thabiti ya usimamizi na udhibiti.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani, Jaji Salma Maghimbi amasema lazima wawe sehemu muhimu kwa kuangalia teknolojia hiyo ili kumlinda mlaji kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.

kongamano hilo limejumuisha wadau na watalaam mbalimbali wakiwemo TEHEMA, Vyuo Vikuu, Taasisi za Utafiti , Afya, Sera na Sheria, pamoja na wafanyabiashara kutoka Sekta Binafsi.



0/Post a Comment/Comments